WAZIRI mkuu wa Australia amesema kuwa mitambo ya satelite ya nchi hiyo imenasa picha za vitu vinavyoonekana kama mabaki ya ndege ya Malaysia iliyopotea siku 13 zilizopita.
Waziri mkuu huyo, Tony Abbott, ameliambia bunge mjini Canberra kwamba picha za Satelite zimeonyesha vitu viwili vinavyofanana na mabaki ya ndege hiyo.
Taarifa hii imejitokeza karibu wiki mbili baada ya ndege hiyo kutoweka na abiria zaidi ya miambili kutoka mjini Kuala Lumpur Malaysia kuelekea Beijing.
Msemaji wa halmashauri ya usalama wa safari za ndege, John Young, baadaye alisema kuwa vifaa hivyo ambavyo kimoja kina ukubwa wa mita 24, vimeonekana umbali wa kilomita 2500 kusini Magharibi mwa pwani ya Australia.
Aliongeza kwamba, itakuwa vigumu kuviona vifaa hivyo na pia huenda sio vya ndege hiyo.
Wakati taarifa hii ilipotolewa, kulikuwa na ndege ya Australia katika eneo hilo, ndege zaidi zinatarajiwa kuwasili katika eneo lenyewe na pia manowari ya jeshi inaelekea huko. (TUKUO)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni