Jumatano, 16 Aprili 2014

ANASWA AKIMNYANYASA MTOTO MDOGO



Mama mmoja maarufu kwa jina la mama Mpare (pichani), mkazi wa Kimara King’ongo jijini Dar es Salaam aliyenaswa kwa kosa la kumtumikisha mwanaye wa miaka 13 kazi nzito.


MAMA mmoja maarufu kwa jina la mama Mpare (pichani), mkazi wa Kimara King’ongo jijini Dar es Salaam amenaswa kwa kosa la kumfanyisha mwanaye kazi nzito zisizoendana na umri wake wa miaka 13 (picha ndogo). Majirani wa mama huyo walitoa taarifa kwa waandishi wetu wakidai kuwa, mwanamke huyo humfanyisha kazi nzito mtoto wake huyo kama mfanyakazi wa ndani akiwatunza wadogo zake huku akiuza genge lililopo karibu na nyumbani kwao.

Mtoto Saumu Shaban (13).


Ilidaiwa kuwa pamoja na kazi hizo ngumu, mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la Saumu Shaban (13) hukaanga chipsi kuanzia mishale ya jioni mpaka usiku wa saa 5 ambapo hufunga shughuli zake kabla ya siku inayofuata kurudia utaratibu huo.

Baada ya kupata taarifa hizo waandishi wetu walifika na kujionea hali halisi ambapo mtoto Saumu alionekana akiuza genge huku vikaango vya chipsi vikionekana tayari kwa ajili ya kupikia mara baada ya jua kuzama.


Akizungumza na waandishi wetu mtoto huyo alikiri kutosoma shule yoyote na kufunguka kuwa yeye ndiye muuzaji wa genge hilo na kwamba baada ya mama yake kufariki ndipo alikuja kuishi na mama yake mdogo.
Waandishi wetu walifika Ofisi za Serikali ya Mtaa wa King’ongo na kutoa taarifa kuhusiana na sakata hilo kwa mwenyekiti wa mtaa huo aliyejitambulisha kwa jina la Demetrius Mapesi ambaye aliongozana na waandishi wetu mpaka kwa mama wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la Saumu Musa.
Akizungumza na waandishi wetu Saumu alisema kuwa Saumu (ambaye ni mtoto anayemtumikisha) ni mtoto wa marehemu dada yake na alimchukua kutoka Tanga kwa ajili ya kumsaidia kazi zake. Alipoulizwa kwa nini hampeleki shule alisema kuwa hana uwezo wa kumlipia gharama za shule mtoto huyo ambapo Mwenyekiti huyo alimtaka ampeleke mtoto huyo ofisini kwake ili aandae utaratibu wa kumpeleka shule.
\NA GPL

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni