Kamishna wa polisi New York William Bratton alikutana na
wakereketwa wa mpango huo
Marekani imefunga kitengo chake
maalum cha ujasusi ambacho huwapepeleza waisilamu ili kuchunguza kama kuna tisho
lolote la ugaidi.
Kitengo hicho kilikuwa kinatumia polisi waliokuwa wanavalia nguo za kiraia
kusikiliza kisiri mawasiliano ya simu kati ya waisilamu na hata kuzuru maeneo
yanayotembelewa sana na waisilamu.
Vyombo vya habari nchini Marekani vinasema kuwa kitengo hicho kiliwahi
kushitakiwa mara mbili kwa mbinu zao za ujasusi na pia kulaaniwa na makundi ya
wanaharakati wa haki za binadamu.
Pia kiliwaghadhabisha waisilamu hasa kwa kuwachunguza.
"mageuzi haya ni hatua muhimu sana katika kuondoa hali ya wasiwasi na
kutoaminiana kati ya polisi na jamii ili jamii iweze kusaidia polisi kuwashika
wahalifu,'' ilisema taarifa kutoka katika ofisi ya meya wa New York Bill de
Blasio.
Hatua ya kusitisha mpango huo, ilifikiwa na kamishna mpya wa polisi wa kituo
hicho, na inaonekana kama njia moja ya kubadili mbinu za kukusanya ujasusi
ambazo wengi wanasema zilichangia mashambulizi ya Septemba 11
Kitengo hicho, kilichoanzishwa mwaka 2003, na baadaye kuitwa, ' Zone
Assessment Unit ' kilipeleleza waisilamu hasa maeneo walikofanya kazi, kuswali,
kununua mahitaji madukani na hata migahawa walikokuwa wanakula.
Wakuu wa kitengo hicho wanasema kuwa kazi yao iliathiri sana uhusiano kati ya
jamii na polisi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni