Ijumaa, 23 Mei 2014

FACEBOOK YAOKOA MAISHA YA MPANDA MLIMA

John All aliyeokolewa na facebook
Mpanda milima mirefu ameokolewa kutoka futi karibu 20,000 bondeni alipoandika ''Nahitaji msaada'' katika mtandao wa Facebook
Profesa huyo wa jiografia aliwaambia marafiki zake wa Facebook kuwa alikuwa ameanguka ndani ya bonde la Himalaya umbali wa futi 19,600 kwenda chini.
Profesa John All aliandika taarifa hii kwenye ukurasa wa facebook wa ‘'American Climber Science Program’' baada ya kuanguka kwenye bonde hilo. All mwenye umri wa miaka 44 aliteguka bega, kuvunja mbavu tano, goti, na kiwiko.
All aliandika, ‘’ tafadhali muwafahamishe waokoaji wa Global, kuwa John amevunjika mkono, mbavu na huenda anavuja damu ndani ya mwili. Tafadhali harakisheni’’
Marafiki wake wa Facebook waliona video ya All akiwa na majeraha na kuwajulisha waokoaji kilichokuwa kikitendeka na kisha kuwasiliana na All na kumwambia kuwa atapata msaada.
Baada ya saa kadhaa, All aliandika kwenye ukurasa huo wa Facebook kuwa waokoaji hawangeweza kumpata kwa kutumia helikopta kwa hivyo angejitahidi ingawa kulikuweko na baridi na alikuwa na maumivu mengi.
Baada ya saa 19, profesa All aliokolewa na kupelekwa hospitalini mjini Kathmandu ambako anapata matibabu(TK)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni