Mkuu wa majeshi nchini Thailand ametangaza mapinduzi akisema
jeshi sasa linachukua udhibiti wa serikali.
Katika taarifa iliyotolewa kupitia kwa televisheni, mkuu huyo wa majeshi
alisema jeshi litarejesha utawala wa kisheria na kufanya mageuzi ya kisiasa.
Majeshi yalizingira eneo la tukio mjini Bangkok ambapo makundi ya kisiasa
yamekuwa yakifanya mazungumzo kwa siku ya pili na kuwachukua viongozi wao.
Mapinduzi haya yanakuja baada ya miezi kadhaa ya ghasia za kisiasa na kuwekwa
kwa sheria ya kijeshi.
Jeshi litatuma vikosi na magari kuwasindikiza waandamanaji kutoka maeneo ya
maandamano, afisa wa kijeshi alilieleza shirika la habari la Reuters.
Ghasia za hivi karibuni zialianza katika mji mkuu wa Thailand mwishoni mwa
mwaka jana, wakati waziri mkuu Yingluck Shinawatra alipovunja bunge la nchi hiyo
.
Waandamanaji waliweka vizuizi kwenye maeneo ya mji wa Bangkok katika kipindi
cha mwezi mmoja.
Mapema mwezi huu , mahakama ilimuamuru kuondolewa madarakani kwa Bi Yingluck
kwa madai ya kutumia vibaya mamlaka.
Thailand imekabiliwa na mzozo wa kupigania mamlaka tangu kaka yake Bi
Yingluck , Thaksin Shinawatra, kung'olewa mamlakani na jeshi kama waziri mkuu
mnamo mwaka 2006 (TK)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni