Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na watanzania
waishio nchini Japan, wakati alipokutana nao kwa mazungumzo yaliyofanyika kwenye
Hoteli ya The New Otani, wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi nchini humo,
jana Mei 21, 2014. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Japan, Salome Sijaona.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Watanzania waishio Japan (Tanzanite Society) David Semiono, akisoma risala ya
Jumuiya yao wakati wa hafla ya chakula cha jioni na Makamu wa Rais Dkt. Bilal,
iliyofanyika kwenye Hoteli ya The New Otan, jijini Tokyo Japan, jana usiku Mei
21, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na watanzania
waishio nchini Japan, wakati alipokutana nao kwa mazungumzo yaliyofanyika kwenye
Hoteli ya The New Otani, wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi nchini humo,
jana Mei 21, 2014. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Japan, Salome Sijaona.
Baadhi ya Watanzania
waishio nchini Japan, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipokuwa wakiwahutubia katika
hafla ya chakula cha jioni, iliyofanyika kwenye Hoteli ya The New Otan, jijini
Tokyo Japan, jana Mei 21, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na mwanamuziki
Mtanzania wa bendi ya The Tanzanite, Abuu Omar, wakati alipokuwa akiagana na
baadhi ya Watanzania waishio Japan, waliohudhuria hafla hiyo ya chakula cha
jioni. Kulia ni Mke wa Makamu, Mama Asha Bilal.
Baadhi ya Watanzania
waishio nchini Japan, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipokuwa wakiwahutubia katika
hafla ya chakula cha jioni, iliyofanyika kwenye Hoteli ya The New Otan, jijini
Tokyo Japan, jana Mei 21, 2014.
Makamu wa Rais Dkt. Bilal
akiwa katika picha ya pamoja na watanzania waishio nchini Japan, baada ya
mazungumzo.
Baadhi ya Watanzania,
waishio nchini Japan wakipiga picha ya kumbukumbu ya pamoja na ujumbe wa Makamu.
Na Mwandishi Maalum –
Tokyo, Japan
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal amewatoa wasiwasi Watanzania
wanaoishi nchini Japan kuhusu mvutano uliojitokeza ndani ya Bunge la Katiba na
kuwahakikishia kuwa ana imani Bunge hilo litakapokutana Agosti mwaka huu mambo
yatakwenda vizuri .
Dkt. Bilal amewatoa hofu
Watanzania hao kufuatia risala yao iliyosomwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo
(Tanzanite Society) David Semiono kueleza masikitiko yao kuhusu kutoridhishwa
na mwenendo wa Bunge la Katiba.
Akizungumza na Watanzania
hao katika ukumbi wa New Otani Hotel hapa Tokyo, Japan jana Mei 21, 2014 Dkt.
Bilal alisema kilichojitokeza katika bunge hilo ni kurekebishana ili nchi iweze
kupata Katiba mpya yenye maslahi kwa wananchi na itakayodumu kwa miaka mingi
ijayo.
Makamu wa Rais alibainisha
kuwa kazi ya kuandika katiba si rahisi kama wengi wanavyofikiria kwani katika
nchi zingine, wanafikia uamuzi huo baada ya kutokea hali ya kutoelewana na hata
kupigana jambo ambalo ni tofauti na Tanzania ambapo uamuzi huo umefikiwa
kiungwana kwa kuheshimu mawazo na maoni ya wananchi wake.
“Sisi kwa salama na amani
tumeanza mchakato wa katiba mpya na tumalize kwa salama na amani, tuendelee na
sifa tuliyonayo ya umoja na mshikamano,” aliasa Dkt. Bilal
Aliutaka Umoja wa Katiba ya
Wananchi (UKAWA) kuacha jazba na kurudi bungeni ifikapo Agosti mwaka huu ili
waweze kushirikiana na wenzao katika kukamilisha kazi hiyo muhimu waliotumwa na
wananchi.
“Tunachoomba waliotoka nje
ya mstari, tusiwe wa kwanza kukaidi na kufuata misingi ya jazba. Tutangulize
kwanza Utanzania wetu. Tunawaomba wote waliotoka bungeni, warudi washirikiane
na wenzao. Tukimaliza kwa amani mchakato huu, tutakuwa tumeijengea sifa kubwa
nchi yetu. Tumeheshimu matakwa ya watu, sote tuheshimu mchakato huu mpaka
tuufikishe mwisho kwa amani,” alisema Makamu wa Rais.
Akizungumzia Muungano,
Makamu wa Rais aliwataka Watanzania hao kuendelea kuuenzi, kuulinda na
kuudumisha kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla, huku akiwakumbusha kuwa muungano
huu umekuwa wakupigiwa mfano Afrika na duniani kwa ujumla.
“Muungano wetu ni
wakujivunia na wa aina yake barani Afrika na kote duniani. Kumbukeni miaka ile
nchi nyingi za Afrika zilijaribu kuungana lakini zilishindwa. Safari ya miungano
yao, ilikuwa fupi na miungano hiyo imesambaratika,” alisema Dkt. Bilal huku
akitolea mfano wa muungano wa senego-Gambia na baadhi ya nchi nyingine za
Kiafrika.
Akijibu malalamiko ya
Watanzania hao waliodai kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) haiwatendei haki
wafanyabiashara wanaoingiza magari nchini kwa kutoza kodi zenye utata bila hata
kuzingatia taratibu zilizowekwa, Dkt. Bilal alisema amelipokea tatizo hilo, na
kufafanua kwamba Serikali inaendelea kuzifanyia kazi kero mbalimbali ndani ya
mamlaka hiyo.
Aliwataka Watanzania hao
kuwa na subra kwani alisema kila jambo huanza kwa hatua moja na halimaliziki kwa
siku moja na kuwahakikishia kwamba anaamini kutokana na juhudi kubwa
zinazofanywa na serikali kero hizo zitapatiwa ufumbuzi haraka.Kuhusu ongezeko la
matumizi ya dawa za kulevya, Dkt. Bilal aliiasa jamii na viongozi wa dini
mbalimbali nchini kushirikiana na serikali kwa kuwapa miongozo ya maadili mema
vijana ili kuepukana na janga hilo na hivyo Taifa liweze kupiga hatua ya
maendeleo.
“Tusifanye mzaha katika
malezi ya watoto wetu, viongozi wa dini zote nchini wana wajibu wa kuwafundisha
vijana wetu maadili mema na sisi wazazi tusichoke kuwakanya vijana wetu kwa
ukali kuhusu matumizi ya dawa za kulevya”, alisema Dkt. Bilal. Makamu wa Rais
alitumia fursa hiyo pia kuhimiza Watanzania kutumia nafasi yao ughaibuni
kushawishi wawekezaji kuja kuwekeza nyumbani kwani Tanzania haiwezi kuendelea
bila kuwa na uwekezaji wa kutosha(TK)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni