Mtoto aliyeunguzwa moto
Wakati Afrika ikadhimisha siku ya mtoto wa Afrika ambayo huadhimishwa kila mwaka Mtoto mmoja wa miaka nane, mkazi wa Mjimwema Songea mkoani Ruvuma amefanyiwa ukatili wa kutisha na Baba yake wa kambo (jina tunalo) kwa kumchoma moto mikono yake yote miwili kwa kosa la kuchelewa kurudi nyumbani.
Jeshi la polisi mkoani Ruvuma bado linamsaka mtuhumiwa wa unyama huo, ambaye alitoroka baada ya kufanya unyama huo huku mtoto huyo akiwa amelazawa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma Songea.
Tukio hilo la kinyama limewafanya baadhi ya madaktari na manesi wa hospitali hiyo kumwaga machozi kutokana na mtoto huyo kufanyiwa kitendo hicho cha kusikitisha cha kuchomwa moto mikono yake miwili na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake.
Afisa muuguzi msaidizi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma anasema mtoto huyo ameumia katika jicho la kulia, mgongoni huku akiwa na majeraha makubwa katika viganja vya mikono yake miwili ambayo alimwagiwa mafuta ya taa na kuchomwa moto (TK)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni