Ijumaa, 27 Juni 2014

SUARES MNG'ATA MENO AZIDI KUUMBUKA MDHAMINI WAKE AJITOA

Mshambuliaji wa timu ya Uruguay Luis Suarez amempoteza mmoja wa wadhamini wake baada ya kupigwa marufuku kwa kumng'ata mchezaji wa Italy Giorgio Chiellini.

Kampuni ya kamari ya mtandaoni 888 poker imesema ''imeamua kusitisha mkataba wake na mchezaji huo mara moja''.

''Kila mtu anajua ni nini alichofanya Luis.

Walitaka aondolewe katika michuano ya kombe la dunia. Na kweli walifanikiwa.

''Walimuondoa katika mechi hizo kama mbwa'' alisema Lila Piris Da Rosa bibiye Suarez.

''Mchezaji huyo wa miaka 27 anayeichezea kilabu ya Liverpool alipigwa marufuku ya miezi minne na shirikisho la soka duniani FIFA baada ya kupatikana na hatia ya kumng'ata Chiellini katika mechi ya kombe la dunia.
"
Suarez hawezi kuchezea kilabu yoyote ama taifa lake hadi mwisho wa mwezi Oktoba.

Atakosa kushiriki katika mechi zilizosalia katika kombe la dunia nchini Brazil.

Uruguay itacheza na Colombia katika mechi za kumi na sita bora siku ya jumamosi baada ya kufuzu katika kundi la 'Da' nyuma ya Costa Rica.

Suarez alijiunga na kampuni ya 888poker kama mjumbe wake duniani siku chache kabla ya kuanza kwa michuano ya kombe la dunia na kutoa baadhi ya kanda za video za shajara ya mtandao wake ikiwemo moja ya bao lake wakati wa ushindi wa taifa lake dhidi ya Uingereza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni