Richard Musya Mwanzia aliyehikumiwa kifo kwa wizi wa kutumia nguvu na kumbaka jirani yake baada ya kuaciwa huru [Photo: File/Standard] |
Richard Musya Mwanzia alipoteza miak 8 ya ujana wake gerezani kutokana na hukumu mbovu iliyomsababishia mateso makali pamoja na kumuathiri kisaikolojia.
Mwaka 2005 bwana Mwanzia alituhumiwa na jirani yake kwamba alimbaka na kumwibia kwa kutumia nguvu. Alikamtwa na kushitakiwa na hatimaye kuhukumiwa kifo. Alifungwa katika gereza la Kamiti (Kamiti Maximum Prison). Kumbe hakutenda kosa hilo ila alihukumiwa kifo na mahakama ya Kitui kutokana na umaskini alishindwa kuweka mwanasheria wa kumtetea. Madai ya kubaka yaliondolewa baada ya mahakama kugundua kuwa hakuwa na uwezo wa kubaka kutokana na kuwa na jinsi mbili.
"Huwezi kuamini jinsi maisha yanavyoweza kuwendea kombo mtu" alisema Mwanzia. Jirani yake Mwanzia aitwaye Belita Musangi ndiye aliyekuwa jirani yake huko Mwambale, Kitui na aliyemtuhumu baada ya watu watatu kuvunja nyumba yake usiku wa kuamkia tarehe 12,9,2005 na kudai awape fedha ambapo alitoa sh za Kenya 16,971 (sawa na sh za Tanzania 320,000. Bwana Mwanzia alikamatwa pamoja na shemeji yake Bwana Kitonga na kuwekwa katika Gereza la Kamiti akingojea kunyongwa. Baadaye aliambiwa kuwa shemeji yake huyo alifariki dunia kutokana majeraha aliyoyapata alipokuwa akipambana na maaskari-jela mwaka wa 2009
.
Baadaye Mwanzia alipata usaidizi wa shirika la kutetea haki za binadamu ambao walimsaidia kukata rufaa na kwenye rufaa hiyo alishinda na kuachiwa huru.
Baadaye Mwanzia alipata usaidizi wa shirika la kutetea haki za binadamu ambao walimsaidia kukata rufaa na kwenye rufaa hiyo alishinda na kuachiwa huru.
“Sina uhakika kama nitaweza maishani kumsamehe Belita kwa mambo aliyonifanyia,” alisema Mwanzia baada ya kutoka jela.
Kesi hiyo iliendeshwa na majaji Hatari Waweru, Jessie Lesiit na George Dulu baada ya Belita kushinda kuishawishi mahaka kama alimuona Mwanzia.
Akiwa gerezani Kamiti, Mwanzia alifungu kesi ya madai ya kudhalilishwa na serikali baada ya kuwekwa gereza la wanaume wakati ana jinjia mbili jambo ambalo lilimfedhehesha sana. Alishinda kesi na serikali kutakiwa kumlipa sh 500,000 ambazo hajalipwa hadi leo (TK).

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni