Dereva Hamidu Juma aliyedai kupigwa na Polisi
DEREVA mmoja wa basi la Princes Munaa linalofanya safari zake Mwanza-Dar, Bw. Hamidu Juma anadai kupigwa na Polisi Juni 26 mwaka huu huko Mbezi, Kimara jijini Dar. Akizungumza na mwandishi wetu, Hamidu alisema “Basi letu lina madereva wawili, zamu yangu ilikuwa imeisha, tulipofika Kimara tulikuta foleni, nikaamua kushuka ili kutazama sababu ni nini, niliporudi nikakuta basi letu liko pembeni likiwa limezungukwa na askari, baadhi wakiwa na nguo za kawaida, walitaka kung’oa karatasi za bima na zinginezo nikakataa ndipo wakadai nawafundisha kazi, wakaanza kunipiga mpaka mifupa ya mkononi imepishana’’.
Aidha dereva huyo anadai hajavunjika ila mifupa imepishana na pia ana uvimbe kwa hiyo amepewa siku saba ndipo arudi kufanyia uchunguzi wa kina.
Hali hii ni hadi lini ya wanaosimamia usalama kuvunja sheria?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni