Jumanne, 1 Julai 2014

MWANAMKE AVUA NGUO MAHAKAMANI KENYA

kny
Hizi ni stori ambazo ukizisikia unaweza kushtuka kuona mtu anawezaje, sasa Unaambiwa kutoka katika mahakama kuu jijini Eldoret Nchini Kenya kuna mwanamke aliamua kuvua nguo ili kupinga uamuzi wa jaji kwenye kesi yake. Kesi iliyokuwa ikimkabili mwanamke huyo ilikuwa ikuhusu mzozo wa ardhi dhidi yake na mwanamke mwingine ambapo wawili hao waliripotiwa kuoana na kwa mujibu wa desturi na mila za jamii ya wa Nandi inamruhusu mke kumuoa mke mwingine. Mila hiyo huwa inazingatiwa endapo mwanamke aliyeolewa ameshindwa kupata watoto au kubainika kuwa tasa na pengine anahitaji kuendeleza kizazi katika familia aliyoolewa, hivyo mwanamke anayeolewa na mke mwingine haruhusiwi kuwa na uhusiano na mke aliyemuoa bali atatafuta mume atakayezaa naye watoto.

Kwenye kesi Hakimu Silah Munyao alikubaliana na hoja ya mlalamikaji kuwa hakukuwa na ndoa na akatoa ruhusa ya kutimuliwa kwa mshtakiwa Hellen Tum [mkewe Tapkili Metto] kutoka kwa shamba hilo na kufidiwa.
Kwenye kesi iliyowasilishwa mahakamani mwaka wa 2005, Tum alikuwa amemshtaki mumewe Tapkili Metto kwa kumkana licha ya kuishi naye kama mume na mke tangu mwaka 1989.
Hata hivyo Tapkili alikataa kuoana na Tum, Akiongeza kwamba yeye alikuwa msaidizi wa nyumba tu yaani Housegirl, hakimu Munyao amesema hajaridhika na mashtaka kwa upande wa mshtakiwa kwamba watoto ambao Tum alimzalia Tapkili kwa kuwa hakukuwa na yeyote alisema alishuhudia ndoa baina ya wake hao wawili.
Muda mfupi baada ya uamuzi wa mahakama Bi Tum alivua nguo nje ya mahakama huku akimtukana hakimu kwa sauti ya juu kabla ya wapita njia kumtaka atulie.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni