Jumatatu, 28 Julai 2014

DEREVA WA BODABODA AKWAPUA SIMU ANUSURIKA KIFO

Dereva wa bodaboda anayetambulika kwa jina la Abuu Athumani (28) mara baada ya kunaswa kwa wizi wa simu.

Ule mchezo wa kukwapua vitu na kukimbia umemtokea puani dereva wa pikipiki almaarufu bodaboda aliyetambulika kwa jina la Abuu Athumani (28) ambaye amenusa kifo baada ya kukwapua simu ya bei mbaya ya mrembo aitwaye Zaituni Hamisi. Tukio hilo la aina yake lilijiri majira ya asubuhi wikiendi iliyopita maeneo ya Sinza-Mapambano, Dar ambapo kwa mujibu wa mashuhuda bodaboda huyo alikuwa amempakiza mwenzake kisha kumfuatilia mrembo huyo kwa nyuma wakati akitembea kwa miguu pembezoni mwa Barabara ya Shekilango.

Dereva huyo wa bodaboda akiwa kwenye mtaro na pikipiki yake mara baada ya kipigo kutoka kwa wananchi.
Shuhuda huyo alisema kuwa alishangaa kumuona yule jamaa aliyepakizwa akimkwapua mrembo huyo lakini kwa bahati nzuri mmoja wa madereva wa Bajaj aliyekuwa karibu alimuona na kumbananisha pembezoni mwa barabara na hatimaye kuingia mtaroni.Raia walioshuhudia mkasa huo wakiitoa bodaboda kutoka mtaroni.
Ndani ya dakika sifuri, yule mkwapuaji alitoka nduki huku akimwacha bodaboda huyo aliyekiona cha moto.Kulia ni mrembo (Zaituni Hamisi) aliyekwapuliwa simu yake na waendesha bodaboda hao.
Alisema ghafla umati ulijaa na kushuhudiwa akipewa kipondo cha kufa mtu na wengine wakidai kuwa ni kawaida ya jamaa huyo kukwapua mikoba ya watu. Baadhi ya watu walikuwa wakichanga fedha kwa ajili ya kununua mafuta ya petroli ili wamchome moto bila kujali polisi aliyefika ambaye alikuwa akijitahidi kutuliza ghasia hizo.
Dereva huyo wa bodaboda akichukuliwa na Polisi mara baada kunusullika kifo kutoka wa raia wenye hasira kali.
Wakati akipewa kipigo, njemba huyo alikuwa akilalamika na kuwaomba wananchi wasimuue kwani amekoma na hatarudia tena.Hata hivyo, bodaboda huyo alinusurika baada ya polisi wa Kituo cha Kijitonyama (Mabatini) kufika eneo hilo kisha kumchukua jamaa huyo na mlalamikaji kwa ajili ya hatua za kisheria.
Imeandaliwa na Chande Abdallah,

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni