Vikosi vya zima moto vya Libya vikipambana kujaribu kuuzima
moto.
Kombora la roketi limelipua tanki la kuhifadhia mafuta wakati wa
mapigano kati ya makundi mawili yanayohasimiana katika mji mkuu Tripoli. Tanki
hilo ni miongoni mwa matanki yanayomilikiwa na Kampuni ya mafuta ya serikali ya
Libya yenye lita milioni sita za mafuta.
Msemaji wa Kampuni hiyo Mohamed
Al-Hariri amesema iwapo moto huo utasambaa kwenye matanki mengine ya karibu
huenda ukasababisha madhara makubwa katika eneo lenye upana wa kilomita tano.
Serikali ya muda ya Libya imetaka usitishaji wa mapigano katika eneo hilo la
maafa ili kuruhusu vikosi vya zima moto kufanya kazi yao bila
kuingiliwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni