Jeshi la Nigeria likiwa katika doria katika
jimbo la Borno nchini Nigeria
Jeshi la Nigeria limepiga marufuku utumizi wa magari kwa siku
tatu katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa taifa hilo ili kuzuia tishio
la wanamgambo wa Boko Haram.
Msemaji wa jeshi amesema kuwa hatua hiyo itazuia utumiaji wa magari
kutekeleza mashambulizi ya kujitolea mhanga wakati wa siku kuu ya Eid ul
Fitr.
Wakati huohuo kumekuwa na ripoti ambapo mlipuaji wa kujitolea muhanga amewaua
watu kadhaa katika mji wa kazkazini wa KANO.
Kundi la Boko Haram limetishia kulipua bomu la
gari
Mwandishi wa BBC Tomi Oladipo anasema kuwa Wanajeshi hao waliwashauri
waislamu kuhudhuria swala za Eid karibu na viwanja vilivyopo karibu na makaazi
yao kwa kuwa kundi hilo lilikuwa linapanga kutekeleza mashambulizi katika
viwanja,masoko pamoja na maeneo mengine ya uma wakitumia magari.
Gavana wa Borno Kassim Shetima amesema kuwa anawaonea huruma maelfu ya watu
waliolazimika kutumia mda wao mwingi kutembea hadi katika viwanja vya kufanyia
salah,lakini akaongezea kuwa hatua hiyo inalenga kuwalinda .
Jeshi la Nigeria limepiga marufuku utumizi wa magari katika
jimbo la Borno
Kundi la Boko haram linadaiwa kuiteka miji kadhaa kusini mwa Borno na kuweka
bendera zake.
Jeshi la Nigeria hivi majuzi lilikiri kwamba baadhi ya wanajeshi wake
walikuwa wanatoroka kutokana na uvamizi wa wanamgambo hao (TK).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni