Polisi nchini Marekani wameshindwa kumkamata balozi wa
Equatorial Guine mjini Washngton, kwa tuhuma za kumpiga binti yake kwa mguu wa
kiti cha mbao, balozi huyo hajakamatwa mpaka sasa kutokana na kinga yake ya
kibalozi aliyonayo .
Msemaji wa polisi Dustin Sternbeck amesema kwamba walipewa taarifa mapema
wiki hii kuwa kuna tukio nyumbani kwa balozi huyo, na walipofika wakamkuta binti
huyo mdogo akiwa na jeraha kubwa kichwani mwake ambaye alihitaji tiba na hivyo
kumpeleka hospitalini kwa matibabu.
Pamoja na hayo yote Dustin alisema kuwa polisi hawana mamlaka kwa kesi za
namna hiyo zinazowahusisha wanadiplomasia lakini wamekwisha iarifu serikali juu
ya suala hilo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni