Jumamosi, 16 Agosti 2014

KITUO CHA KUPOOZEA UMEME CHAUNGUA MJINI MOSHI




Askari wa kikosi cha Zimamoto wakifika eneo la tukio asubuhi hii

Wananchi wakishuhudia juhudi za kuzima moto huo



Moto ukiendelea
Juhudi zikiendelea. Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Transforma zinazosambaza umeme katika maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi Mkoani Kilimanjaro zilizoko eneo la Bomambuzi zimewaka moto asubuhi hii muda mfupi baada ya kutokea shoti ambayo haijafahamika chanzo chake ni nini.
Moto huo umetokea majira ya saa 1:10 na kusababisha maeneo kadhaa ya mji wa Moshi kukosa umeme hadi sasa.
Globu ya jamii imeshuhudia kikosi cha zimamoto kutoka manispaa ya moshi kikijaribu kuzima moto huo ambao hata hivyo ulikwisha teketeza sehemu kubwa ya kituo hicho cha kupozea umeme.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni