Abiria wawili wa china waliokuwa wakisafiri na ndege ya shirika
la ndege la China (China Airline), wameamua kulipeleka shirika hilo mahakamani
kwa kile walichokieleza kuwazuia kusafiri na shirika hilo eti tu kwasababu
walikua wanaishi na virusi vya ukimwi HIV.
Hata hivyo inaelezwa kwamba abiria hao si mara ya kwanza kusafiri na China
Airline kutoka kaskazini mwa mji wa Shenyang katika kipindi cha machipuko
,wakati huu sasa shirika hilo la ndege lilipoamua kughairisha safari za abiria
hao.Masharti ambayo abiria hao wameyatoa Kufuatia kughairishwa kwa safari hiyo,shirika hilo la ndege litalazimika kuomba radhi na kulipa fidia ya dola za kimarekani elfu nane .Mahakama katika mji wa Shenyang imeipokea na kukubali kesi hiyo ya kwanza na ya kipekee nchini China.
Viongozi wa serikali kutoka China wamesema kua wamejitahidi kujaribu kupunguza historia ya muda mrefu ya unyanyapaa kwa wanaoishi na virusi vya HIV na ukimwi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni