Mapiganao makali yamezuka katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.
Hi ni baada ya vikosi vya serikali kuzindua oparesheni leo alfajiri dhidi ya
nyumba moja inayomilikiwa na mbabe mmoja wa kivita kama kampeni ya vikosi hivyo
kuwapokonya silaha wapiganaji.Vikosi vya serikali vinasema kuwa vimeiteka nyumba hiyo ya Ahmed Dai katika oparesheni iliochukua zaidi ya saa tano.
Ahmed Dai alifanikiwa kutoroka, lakini wapiganaji kadhaa wa kundi lake walikamatwa na silaha zao kuchukuliwa.
Ameambia BBC kwamba ametoroka baada ya wanajeshi wa serikali kuanzisha operesheni kali dhidi yake na wapiganaji wake.
Ahmed Dai huongoza kikosi kikubwa cha wpaiganaji ambao muda wote hutoa ulinzi wa wageni.
Hata hivyo amesema kuwa ataendelea kupigana na kwamba alitumia silaha hizo kujilinda.
Wapiganaji wake walikuwa wakitekeleza oparesheni zao karibu na eneo la uwanja wa ndege linalolindwa sana.
Oparesheni hiyo ya kuwapokonya wapiganaji silkaha ilianza wiki iliopita na serikali inasema kuwa imefanikiwa kupata bunduki 500 pamoja risasi.
Takwimu zinasema kuwa kuna zaidi ya bunduki nusu millioni katika mikono ya raia nchini Somalia ambako sheria hazifuatwi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni