Jumapili, 17 Agosti 2014

MAN U YAANZA LIGI KWA KIPIGO KUTOKA SWANSEA

Kweli Kocha Louis van Gaal ameanza na mguu mbaya maana Man United imefungwa mabao 2-1 na Swansea, lakini kibaya zaidi ni kupoteza mechi ya kwanza ya ligi.Man United ilikuwa haijapoteza mechi ya ugenini tokea mwaka 1972, lakini mzigo wa kuivuruga rekodi hiyo umeangukia van Gaal.

Hata David Moyes ambaye aliboronga msimu uliopita, alijitahidi na kushinda mechi ya kwanza ya msimu.
Baadhi ya mashabiki wa Man United wameonyesha hawana subira na kusema van Gaal amewakera.
Lakini Mholanzi huyo amejibu kwa kusema kikosi chake hakikucheza kitimu na yeye ndiye anawajibika.

Mchezaji  wa Manchester United Wayne Rooney akishangilia bao

Wachezaji wa Swansea wakishangilia bao la ushindi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni