Watu wawili wamefariki dunia papo hapo baada ya gari aina ya Land Cruser ilikuwa imebeba maiti 10 zikitokea hospitali ya Taifa Muhimbili kwenda hospitali ya St Francis Ifakara kugonga wapanda pikipiki katika eneo la Mtego wa simba Mikese mkoani Morogoro
Gari lililosababisha ajali toyota Land Cruser
Mwili wa mmoja waliofariki katika ajali hiyo
Pikipiki iliyosababishiwa ajali na kutoa uhai wa watu wawili waliokuwa wanakwenda shamba
Akizungumzia tukio hilo kwenye eneo la tukio mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Bonifas Mbao amesema gari hiyo ikiendeshwa na dereva Pankrasi Pasco mkazi wa ifakara iliwagonga wapanda pikipiki Shaban Rajab na Ally Benulo wakazi wa Mikese na kufariki dunia papo hapo na chanzo cha ajali mwendo kasi na dereva anashikiliwa na jeshi la polisi. Kuhusu maiti 10 zilizokuwemo katika gari hiyo amesema zilikuwa zikipelekwa hospitli ya St Fancis Ifakara kwa lengo la kufanya utafiti na mafunzo ambapo wanafanya mawasilino ya kuzifikisha katika hospitali hiyo.
Nao wananchi walioshuhudia tukio hilo wameeleleza chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi huku wakilalamikia matukio ya ajali nyingi katika eneo hilo kutokana na kona na kuomba serikali kuweka matuta na vibao vya tahadhari (TK)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni