Kampenzi
kubwa imezinduliwa nchini Tanzania, ikiongozwa na Raisi Jakaya
Kikwete, kutafuta fedha kwa ajili ya kuwalinda watu wenye ulemavu wa
ngozi maarufu kama albino. Katika
miaka ya hivi karibuni, nchi hiyo imekuwa na matukio mengi ya mauaji ya
albino kwa imani za kishirikina huku wahusika wakiamini kwamba viungo
vya walemavu hao vinaweza kuwapatia utajiri.
Pesa itakayokusanywa kutokana na kampeni hiyo, itatumika katika elimu kwa umma .
Mwandishi wa BBC Salim kikeke anaarifu kutoka mjini Mwanza kaskazini mashariki mwa Tanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni