Ijumaa, 29 Agosti 2014

RONALDO MCHEZAJI BORA ULAYA

RONALDO_0109c.jpg
Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Uefa, na kuwapiku kipa wa Bayern Munich, Manuel Neuer na Arjen Robben.

Ronaldo, 29, kutoka Ureno alipachika mabao 17 na kuisaidia Real Madrid kunyakua Kombe la Klabu Bingwa Ulaya - Uefa Champions League- msimu uliopita.
"Nimefurahi sana, kwa hiyo lazima niwashukuru wachezaji wenzangu kwa sababu bila timu, tuzo binafsi ni vigumu kuzipata." Amesema Ronaldo.

Ronaldo aliwazidi Neuer na Robben katika kura zilizopigwa na jopo la waandishi wa habari 54.
Neuer, 28, aliisaidia Ujerumani kushinda Kombe la Dunia, huku Robben, 30, akifunga magoli 21 ya Bayern na matatu kwa timu ya taifa ya Uholanzi iliyofika nusu fainali Brazil.
Ronaldo alifunga mabao matatu - hat-trick - wakati Ureno ilipoichapa Sweden katika mchezo wa kufuzu kucheza Kombe la Dunia, ingawa hakuweza kuwika Brazil, kwani Ureno ilitolewa katika ngazi ya makundi.
Hata hivyo, kiwango chake katika ngazi ya klabu kiliweza kushawishi jopo lililopiga kura, ambalo lilitakiwa kuchagua mshindi kati ya watatu hao baada ya mchujo kutoka wachezaji 10

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni