Alhamisi, 28 Agosti 2014

SIKUSHANGAZWA NA KIPIGO CHA MBWA: ASEMA VAN GAAL KOCHA WA MAN U


Sikushangaa kulazwa4-0 na MK Dons
Kocha wa Manchester United Louis van Gaal amewaudhi wapenzi wa klabu hiyo baada ya kusema kuwa hakushangazwa na kichapo cha mabao 4-0 mikononi mwa klabu ya daraja la kwanza MK Dons katika mechi ya kuwania ubingwa wa kombe la Capital One .
Man U ilibwagwa nje ya kipute hicho baada ya kushindwa katika mechi tatu za kwanza akiwa mkufunzi.
''mimi sishangazwi na matokeo hayo kwa sababu najua kilichofanyika .
''Timu haijengwi kwa mwezi mmoja''
" Milton Keynes walicheza vizuri sana na pia walikuwa na bahati nzuri walipofika mbele ya lango"
Katika mechi hiyo Jonny Evans alifanya makosa na kumruhusu Will Grigg kufungua mvua hiyo ya mabao .
Grigg alifanya mabao kuwa mawili kwa nunge kunako dakika ya 60 ya kipindi cha pili kabla ya mchezaji wa Arsenal aliyeko huko kwa mkopo Benik Afobe kufumania nyavu mara mbili na kuzamisha matumaini yeyote ya Man U kukomboa mechi hiyo.
Van Gaal alisema kuwa alikuwa anataka kujua uwezo wa kikosi chake cha pili haswa baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Sunderland wikiendi iliyopita.
Nilikuwa nawajaribu wachezaji wetu wa timu ya pili
''Najua tulifanya makosa mengi mno lakini tena unajua ilikuwa ni jaribio''
"nilibadilisha mfumo na nikawataka wachezaji mmoja mmoja ili niweze kusaili uwezo wao lakini unaona kilichotokea .''
''Tulicheza vyema na kupata nafasi nyingi tu lakini haikuwa siku yetu''
Van Gaal alitua Old Trafford baada ya United kumaliza katika nafasi ya 7 katika ligi kuu ya Uingereza na amewanunua wachezaji wengi tu kwa gharama ya pauni milioni 131.7 akiwemo
mchezaji aliyegharimu kitita kikubwa zaidi katika ligi ya Uingereza Angel Di Maria aliyegharimu pauni milioni 59.7 alipotokea Real Madrid .
Kichapo hicho kwa kikosi kilichogharimu chini ya nusu milioni kukiweka pamoja ni ishara ya jinsi hali imezidi kudorora tangu aondoke kocha Alex Fergusson

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni