Hii ni sehemu ya picha ya mafunzo hayo kabla ya tukio.
Pale ambapo kwanza unaweza kushtushwa na umri mdogo wa mtoto mwenyewe aliyekuwa anafundishwa kufyetua risasi kwenye bunduki, hii imetokea Arizona nchini Marekani ambapo mtoto wa miaka 9 ndio kichwa cha habari kwenye mafunzo ya kutumia submachine gun (SMG) iliyotengenezwa Israel.
Mtoto huyu wa kike anayetokea New York alikuwa kwenye mapumziko na matembezi kama mtalii kwenye mji wa Arizona ambako pia ndio alichukuwa time yake ya ziada kujifunza kutumia bunduki lakini kwa bahati mbaya risasi ikafyetuka na kumjeruhi mwalimu wake aitwae Charles Vacca mwenye umri wa miaka 39 ambaye alifariki baadaye hospitalini.
Wakati tukio linatokea mtoto huyu alikuwa na wazazi wake ambapo tovuti ya bullets and burgers imesema watoto kati ya miaka 8 na 17 wanaweza kufyetua risasi kama iwapo tu watakuwa chini ya uangalizi wa Mzazi au Mwalimu.
Hii sio mara ya kwanza kwa tukio kama hili, ilishawahi kutokea mwaka 2008 ambapo mtoto wa miaka 8 alijiua kwa bahati mbaya kwa risasi kwenye onyesho la bunduki hukohuko Marekani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni