Jumanne, 23 Septemba 2014

FAMILIA YA MKENYA ALIYEFUNGWA SAUDI ARABIA YAOMBA SERIKALI ISAIDE ATOKE

KIAMBU: Familia moja kutoka kijiji cha Gitothua, Ruiru nchini Kenya imeiomba serikali ya nchi hiyo kuingilia kati suala hilo ili ndugu yao anayeshikiliwa katika gereza moja nchini Saudi Arabia aachiliwe na kurejeshwa nyumbani.
Jane Wangari alisema kuwa binti yake aitwaye Virginia Wanja, miaka 24, ambaye alienda nchini Saudi Arabia mwezi Juni mwaka huu ili kupata kazi nzuriamefungwa katika gereza oja huko kwa miezi miwili sasa.
Mama huyo mwenye watoto wanne alisema mwanaye aliahidiwa kupatiwa kazi ya ualimu wa Kompyuta ambapo baadaye iligundulika kuwa ilkuwa ni lugha ya kumlaghai ili aweze kuondoka nchini Kenya.

Alisema kuwa alipofika Saudia aliambiwa kuwa hamna kazi kama hiyo na kuwa alipewa kazi ya kuwa house girl  ambapo alikubali ka shida.

"alipokuwa anaondoka aliahidiwa mshara wa sh za Kenya 24,000 (sawa na sh 480,000 za Kitanzania. Cha kushangaza alipofika tu aliambiwa kuwa atalipwa sh za Kenya 10,000 sawa na sh 200,000 za Kitanzania na hajapewa hata senti moja hadi sasa". alisema mama yake mzazi huku akibubujikwa na machozi kwenye mashavu yake.

Mama huyo alidaimkuw abinti yake mara baada ya kufika alimjulisha kwa simu kuwa anateswa na kupewa kazi nyingi bila chakula.
"Aliniambia kuwa anafnya kazi katika nyumba tatu tofauti bila mshahara wala chakula. Pia alitakiwa kutolala nyumbani kwa mwajiri na kuwa aliruhusiwa kulala siku mbili kwa siku," alisema mama huyo.
Alipochoka na uonevu huu aliamua kukimbilia polisi kuomba msaada ili arudi nyumbani.

Mwajiri wake alifanya mpango na polisi ili ashikiliwe kwa kutroka kwa mwajiri na akapelekwa gereza la Tahrir  ambapo ameshikiliwa hadi sasa.
Mkenya mwingine aitwaye Mary Nzilili kutoka Kilifi ambaye amefanikiwa kurudi nchini Kenya  ilidai kuwa alikuwa ameshikiliwa katika gereza hilohilo akiwa na Virginia alisema kuwa wafanyakazi wa ndani wanateswa sana nchini Saudia  na akawaomba  wanawake wa Wakenya wasikubali kurubuniwa kwenda kuatfuta kazi nje ya nchi hiyo.
Bi Nzilili, ambaye alikaa huko kwa miezi sita alisema alipata mateso hayohayo aliyopata Virginia baada ya kuamua kuacha kazi kutokana na alichoita mateso yasiyosemekana.
"Kuna wanawake wengi kutoka Kenya wanaoteswa nchini Saudi Arabia. Niliacha wanawake 13 wa Kenya katika gereza hilo. Serikali yetu ni lazima iingilie kati suala hilo ilikuwaokoa wanawake hao ambao hawana hatia na wanaozea nchini Saudia" alisema Nzilili.

Hili ni somo tosha kwa wanawake kutoka Tanzania waogope kuahidiwa kazi nchini Saudia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni