Mashuhuda wa ajali hiyo walisema kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa moja asubuhi wakati dereva aliposhindwa kulidhibiti na kusababisha kupinduka likiwa na lita 30,000 za mafuta.
Wakazi wa eneo hilo walianza sherehe ya kuchota mafuta ambayo yalikuwa yakitiririka ovyo kwenye mfereji.
"Nilikuwa dukani kwangu niliposikia sauti ya gari linaloenda kwa kasi likija, na baadaye nikasikia kishindo kikubwa". alisema mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo.
Polisi walifika eneo la tukio mara moja lakini wakajikita vkwenye wakati mgumu kudhibiti kundi kubwa la vijana waliokuwa wakiiba mafuta na hatari ambayo ingewpata endapo lori hilo litawaka moto.
"Polisi walifanikiwa kudhibiti vijana hao na hakuna madhara yaliyotokea,"alisema Bw Mwangi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni