Jumanne, 23 Septemba 2014

TILES ZISIZOTELEZA ZATAMBULISHWA NCHINI

Kampuni ya Canadian Solution Trading&Cleaning Est Juzi imetambulisha Aina Mpya Ya Tiles kwenye soko la Tanzania ikiwa na kauli ya "SURE STEP" ndani ya Hotel ya Double Tree Jijini Dar es Salaam. Aina mpya hiyo ya Tiles ni mpya nchini kwani ni aina ambayo haina utelezi wakati wote hata pindi ikiwa na maji au Imelowa kwa Mvua au Unyevunyevu. Sure Step inafanya Kazi Vipi?akiongea na wageni walioalikwa na wadau mbalimbali Bwana Thomas amesema kuwa Tiles Hizo zina ubora wa hali ya juuu ikiwemo Garantii ya Mwaka Mmoja mpaka Mitatu.P ia akaongeza Tiles hizo pindi zitumikapo haziwezi kuharibu sakafu wala kuweka nyufa, pia ni rahisi kusafisha pindi tu zinapochafuka kwani zimetengenezwa kwa mfumo ambao haziwezi kunyonya uchafu wa aina yoyote ile. Bwana Thomas akaongeza kuwa pia Bidhaa hiyo ni rafiki wa mazingira kwani haina aina yoyote ya kemikali na pia zinaweza kutumika kwa matumizi ya ndani na nje. Aina za Tiles zilizotambulishwa ni pamoja na Stay Clean NS30, Stay Clean NS60 na Stay Clean NS90.
 
Bwana Thomas alisisitiza kuwa nia ya kampuni ya Canadian Solution Trading&Cleaning Est kutambulisha Tiles hizo Nchini ni kuongeza Usalama wa watumiaji wa maeneo mbali mbali ikiwemo Hoteli, Migahawa, Majumbani, sehemu za Burudani na Maofisini Bwana akatoa mfano kuwa Nchini Canada kumekuwa na kesi nyingi za watu kuvunjika miguu kupata maumivu kutokana na matumizi ya Tile ambazo zinateleza Pindi tu zipatapo maji Au unyevu. Hivyo akatoa wito kwa makampuni mbalimbali ya Ujenzi Tanzania na Nje ya Tanzania kutumia Bidhaa zao ambazo ni salama na rafiki kwa matumizi ya Binadamu.
Wakurugenzi wa Kampuni ya Canadian Solution Trading&Cleaning Est Kutoka kulia ni Nale Nat Alyalei akifuatiwa na Mustafa Said, Khadija Naif Alyafa(Mwenyekiti) na Wa mwisho kushoto Naji Ahmed akifuatilia utambulisho wa bidhaaa inayouzwa na kampuni yao.

Mr Thoamas Toka Canadian Solution Trading&Cleaning Est Akielezea namna jinsi moja ya Bidhaa yao ambavyo haishiki maji kwa namna yoyote ile pindi tu inapokuwa imelowa au kupata unyevu
Wageni waalikwa na Wadau wakifuatilia kwa makini Maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Mr Thomas
Wageni waalikwa na Wadau wakifuatilia kwa makini Maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Mr Thomas

Wadau mbalimbali wakiwa makini kusikiliza na Kusoma kila kilichokuwa kinaelezwa na Mr Thoma toka kampuni ya Canadian Solution Trading&Cleaning Est Jana Kwenye Hoteli ya Double Tree Jijini Dar

Mr Thomas toka kampuni ya Canadian Solution Trading&Cleaning Est akionyesha mfano wa kitambaa ambacho ukimwagia maji hakilowi wala kushika maji ikiwa ni kuelezea namna bidhaa zao zilivyo

Wageni waalikwa na Wadau wakiendelea kufuatilia
Mustapha Said Toka kampuni ya Canadian Solution Trading&Cleaning Est akiwakaribisha wageni waalikwa kwenda kwenye meza kuu kujione kwa macho ni namna gani bidhaa zao zinavyofanya kazi.
 Bwana Thomas toka kampuni ya Canadian Solution Trading&Cleaning Est akiwanyesha kwa vitendo wageni waalikwa na wadau mbalimbali namna bidhaa zao zinavyofanya kazi kwenye mazingira tofauti.

Wageni waalikwa Wakiendelea kupata maelezo na kuuliza maswali kwa Bwana Thomas toka kampuni ya Canadian Solution Trading&Cleaning Est jinsi bidhaa zao zilivyo na zina ubora gani

Maelekezo yakiendelea toka kwa Bwana Thomas kwa wageni mablimbali

Wageni mbalimbali na wadau wakijaribu wenyewe ili kuweza kudhibitisha kile alichokuwa anaongea Bwana Thomas kuhusu Tiles zao mpya ambazo hazina utelezi

Wakurugenzi wa kampuni ya Canadian Solution Trading & Cleaning Est kutoka Kushoto ni Chair Woman Khadija Naif Alyafa akifuatiwa na Mustapha Said, Nala Nait Alyafa na wa mwisho Kulia ni Naji Ahmed

Bwana Thomas Ikabidi atoke nje na wageni waalikwa na wadau ili kuweza kuwanyosha kwa uhalisia kabisa namna bidhaa zao zilvyo

Wadau wakijaribu kukanyaga Tiles na Kuona kama Zinateleza ama Vipi ndani ya Hoteli ya Double Tree Jijini Dar wakati wa utambulisho wa Tiles Mpya Toka Kampuni ya Canadian Solution Trading & Cleaning Est

Hii ni Bidhaa iitwayo STay Clean Ceramic

Hii ni Bidhaa iitwayo STay Clean NS90

Hii ni Bidhaa iitwayo STay Clean NS60

Hii ni Bidhaa iitwayo STay Clean NS30

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni