Furahia Mbugi akiwa kitandani
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Iringa TUMAINI MSOWOYA KIBIKI, Alipomjulia hali bwana Mbugi.
NA TUMAINI MSOWOYA KIBIKI
"Karibu dada, naitwa Furahia Mbugi, nikusaidie nini?" Nilisikia sauti kwa mbali, nilipobisha hodi kwenye nyumba moja, kijiji cha Usuka, mkoani Njombe baada ya kupotea nilikokuwa naenda. Lengo ilikuwa nielekezwe njia.
"Sijambo dada, usishangae kukaribishwa mpaka ndani nilikolala kwani sina uwezo wa kuamka ni miaka mitano sasa, mikono inanguvu ila kiwili wili na miguu havina kazi tena, najisaidia na kupata mahitaji muhimu hapa hapa kitandani, hakika hujafa hujaumbika na sijui kama nitarejea hali yangu ya zamani," anasema.

Miaka 22 ya maisha yake, Furahia Mbugi alikuwa mzima na alichangia shughuli za maendeleo kijijini na alikuwa kiungo kikubwa kwa familia yake.
Familia ya mzee Axon Mbugi (68), ilimtegemea kwa kila kitu, kwani ndiye kifungua mimba.
"Nilishakuwa na mchumba, nilitarajia kuoa lakini ndoto hiyo haipo tena, sasa imeshapita miaka mitano naye ameshaolewa, hata angebaki kunitazama mimi sina uwezo wa kumuoa tena," anasema
Tangu apate ajali, miaka mitano iliyopita ndoto za maisha yake zimeyoyoma.
Mwaka 2009, ndio ulikuwa wa majonzi maishani mwake. Aliamka asubuhi kama kawaida, na kuwaaga wazazi wake kwamba anaenda kwenye shughuli zake.
Siku hiyo Mbugi alienda kupakia mchanga kwenye lori katika eneo la bonde la 'Idindili munyo', lililo katika kijiji cha Kihwele karibu kabisa na kijiji chao.
Aliingia kwenye handaki, na kuanza kuchimba mchanga mzuri kwa ajili ya kujengea.
Ghafla alisikia kishindo kizito ambacho kilipoteza fahamu zake. Alipoamka alijikuta katika hospitali ya misheni ya Ilembula, lakini hakuweza hata kuinua mkono wake.
Machozi yalimtoka pale, alipobaini kuwa ameumia kwa kiwango kikubwa na hataamka mapema hivyo alihamishiwa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Iringa ambako alitibiwa na baadae kuruhusiwa kurejea nyumbani baada ya ahueni.
Mpaka sasa hali yake sio nzuri na anahitaji msaada wako ili maisha yake yaendelee.
Mpigie au mtumie chochote kwa simu NAMBA; 0764 797240

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni