Mchezaji wa Man U di Maria akipiga mpira wa adhabu ndogo kutoka mita 35 ambao ulienda moja kwa moja kimiani na kuzaa bao lake la kwanza tangu ajiunge na Man U.
Katika ligi kuu ya England, ushindi wa Manchester United wa mabao 4-0 dhidi ya Queens Park Rangers umempa nguvu meneja wa timu hiyo Luis Van Gaal na kusema kuwa matarajio yake ni kurejesha taji la ligi katika uwanja wao.
Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya mchezo kuisha amesema, "Nataka kushinda taji la ligi kuu, kama si mwaka huu basi msimu ujao na kama sio ujao basi utakaofuata, nataka kuwapa ushindi mashabiki". Van Gaal, akipata nguvu za ushindi.
Pichani di Maria akishangilia goli lake
Hii leo, Hull City wanawaalika West Ham United katika KC Stadium ama Kingston Communications.Kwa bahati mbaya Hull City italazimika kucheza bila mshambuliaji bwana mdogo aliyezaliwa mwaka 1990 Abel Mathías Hernández Platero.
Mshambuliaji huyo kutoka Uruguay ni mmoja wa wale waliosajiliwa katika ile tunayoweza kuiita dakika ya tisini akitokea Palermo lakini mashabiki wa Hull watalazimika kusubiri baada ya meneja Steve Bruce kutangaza kuwa kibali cha kufanya kazi hakijapatikana bado. Pengine atatokea katika mfumo wa kuwashangaza mashabiki. Uzuri ni kuwa Muuruguay mwingine Gastón Ezequiel Ramírez Pereyra atakuwepo katika safu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni