Marekani imetawazwa Mabingwa wa kombe la Dunia wa mchezo wa mpira wa kikapu kwa kuichapa Serbia vikapu 129 kwa 92. Marekani wameutetea ubingwa wao waliouchukua huko Uturuki mwaka 2010.
Angola na Senegal ziliiwakilisha Afrika ingawa hazikufika mbali sana.
Kombe la Dunia la Mpira wa Kikapu la Mwaka huu wa 2014 lilikuwa toleo la 17 la FIBA Basketball World Cup kwa kuwa hapo awali michuano hii ilifahamika kama FIBA World Championship.
Michuano hii iliyofanyika Hispania ni ya mwisho kufanyika katika mzunguko wa miaka mnne kwani michuano ijayo itafanyika miaka mitano ijayo yaani mwaka 2019 ili kurekebisha hesabu za miaka kuingilia ratiba ya Kombe la Dunia na FIFA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni