Alhamisi, 25 Septemba 2014

MAJAMBAZI YAWATUPIA PESA WATU WALIOKUWA WAKIWAFUKUZA WAFANIKIWA KUTOROKA

Nairobi, Kenya: Kituko kilitokea mtaa wa Banda jijini, Nairobi leo baada ya majambazi wenye silaha walipowarushia fedha wananchi wenye hasira na kufanikiwa kutoroka kwenye duka la  Mpesa ambapo walikuwa wamepora sh milioni 1.4 za kenya sawa na milioni 20 za kitanzania.

 Majambazi hayo manne yaliyokuwa na bastola walivamia duka hilo la Mpesa lililoko kwenye ghorofa ya chini ya Gilfilan House yalipora fedha hizo na kisha kuanza kuondoka kwa miguu.
Mhudumu wa duka hilo alamua kuwafukuza huku akiomba msaada kwa wananchi.

Mashuhuda wa tukio hilo alidai kuwa aliona jambazi mmoja akiwa ameshikiliwa na wananchi hao waliokuwa na kiu kubwa ya kumwaga damu yake karibu na msikiti wa Jamia.

Ilibidi achukue bunda la noti katika mkoba aliokuwa ameweka hela hizo na kwatupia wananchi hao. .
Wananchi hao walipoona noti zile walimwacha na kuanza kugombania noti zile ingawa mama huyo mhudumu wa duka aliendelea kugutia mwizi.
Mama huyo, Shaheen Afzal, aliendelea kuwafukuza huku akipiga kelele za mwizi ambapo baada ya mita 50 jambazi mwingine alitupa noti karibu na  Bazaar Plaza kitu ambacho kilifanya wananchi waache kuwakimbiza na kwenda  kugombania pesa hiyo na wao kufanikiwa kutoroka.

Shaheen lisema kuwa majambazi hayo pia yalidondosha pochi yake waliyoiba pale dukani na kuchanyikana na raia waliokuwa wanatembe barabara ya Moi na kutoweka.

Baba yake Shaheen aitwaye Mohamed Afzal alosema kuwa majambazi hayo yaliingia dukani kwake saa 5 wakijifanya wanunuzi na kuwa walitaka kutuma pesa.
“Mmoja wao alikuja na kuketi akijifanya ni mteja ndipo wale watatu walipfika na kuanza kutuvuruga. Mmoja alisimama mlangoni na kuzuia wateja kuingia,” alisema Afzal.
Afzal alisema kuwa walivunja makabati na kuchukua hela hizo zilizokuwa tayari kupelekwa benki.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni