Alhamisi, 25 Septemba 2014

WALINZI NA POLISI WANYANG"ANYWA SILAHA ILI KUZIPIMA

Kenya: Walinzi  wawili ( bodyguards) ambao walikuwepo eneo la Bunge la  Makueni siku ya Jumanne ambapo yalitokea majibizano ya risasi wamenyang'anywa silaha zao.

Bunduki zao pamoja na risasi 8zimepelekwa kwa mako makuu ya Upelezi ili kuainisha ni silaha gani iliyohusika katika vurugu hizo.

 

Pamoja nao Askari polisi watano waliokuwa eneo hilo nao wamenyang'anywa silaha zao.

 

Mkurugenzi wa Upelelezi bwana Ndegwa Muhoro alisema kuwa wanataka kujua ni silaha gani zilitumika kabla ya kuchukua hatua kali.

 

Alisema kuwa uchunguzi wa awali unaonesha kuwa kulikuwa na uzembe katika matumizi ya silaha za moto.

"Silaha hizo zinafanyiwa uchunguzi katika uchungu wetuwa tukio hilo. Hata hivyo imeonekana wazi kuwa kulikuwa na matumizi mabaya ya silaha na tunataka kupata ushahidi wa kina kuhusu jambo hilo," Alisema.

Aliongeza kuwa Mkuu wa CID  Nyeri Bwana Mohamed Amin ndiye anayeongoza timu ya wapelelezi kutoka Nairobi kuchunguza wa tukio hilo la aibu.

"Zama za uhuni wa aina hii zimepita na watu wanapaswa kujua kuwa mambo yameebadilika.," alisema Muhoro.

Watu sita walijeruhiwa katika tukio hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni