Marekani yatinga fainali kombe la dunia mpira wa kikapu kwa kuiangushia kichapo Lithuania.
Fainali za kombe la dunia la mpira wa kikapu zinaendelea huko nchini Hispania. Timu ya Marekani jana ilitinga fainali hizo kwa kuifunga Lithuania vikapu 96 kwa 68.
Hivyo kwa ushindi huo mnono Marekani sasa inaisubiri mshindi kati ya Ufaransa na Serbia zitakazopambana baadaye leo.
Lithuania inamsubiri atakayopoteza katika mechi hiyo ili kutafuta mshindi wa tatu kesho huku fainali yenyewe ikisubiriwa Jumapili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni