Ijumaa, 12 Septemba 2014

MCHEZAJI MAARUFU WA MIELEKA WWE SEAN O'HAIRE AMEFARIKI DUNIA

Sean O'Haire (kushoto)
Aliyekuwa mchezaji mahiri wa mieleka wa WWE bwana Sean O'Haire amekutwa amefia nyumbani kwake nchini Marekani.

Sababu ya kifo cha mcheza mieleka huyo ambaye alikuwa na umri wa miaka 43 hakijafahamika. Polisi wamesema haukuna mtu wanayemtilia shaka baada ya kukagua nyumbani kwa marehemu mjini South Carolina.

Kifo cha Sean ni mojawapo ya vifo vingi vya mapema vya wacheza mieleka.

O’Haire ambaye jina lake kamili ni Sean Haire - alianza kutengeneza jina kwenye mieleka iliyokuwa inaitwa WCW in 2000 ambayo haipo kwa sasa. Alikuwa akishirikiana na mwenzake Chuck Palumbo.

Alikuja kupata umaarufu baada ya kujiunga na WWE, ambao walimpatia umaarufu mkubwa.

Alikuwa na urefu wa futi 6 na inchi 6 na alikuwa na kipaji kikubwa sana katika mieleka. ingawa hakuwahi kuwa bingwa dunia kwenye fani hiyo ya mieleka.

Vifo vya wacheza mieleka vinatisha ambapo kuanzia mwaka 1990 zaidi ya wachezaji 200 wamefariki hadi sasa. 

Mwezi Aprili mwaka huu mchezaji mwingine mahri aliyejulikana kama  The Ultimate Warrior alifariki dunia masaa kadhaa baada ya kuwaambia maelfu ya mashabiki wake kuwa "Kila mtu moyo wake utapiga pigo la mwisho”.
Mchezaji mwingine maarufu James Hellwig (miaka 54), alikuwa anarejea hotelini kwake huko Arizona alipofarikighafla mbele ya mke wake aitwaye Dana.

Walimfanyia postmortem walisema kifo chake kimetokana na moyo kusimama ghafla (heart attack)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni