Jumatano, 10 Septemba 2014

UTAIFA WA LIBERIA NA EBOLA NGOMA NZITO

Liberia inasemekana kuwa na changamoto za miundo mbinu kuweza kukabiliana na Ebola
Liberia inakabiliwa na tisho kubwa kwa utaifa wake huku janga la Ebola likiendelea kuenea kwa kasi kubwa nchini humo.
Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya waziri wa ulinzi nchini humo.
Brownie Samukai aliambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, kwamba juhudi za kimataifa za kupambana na ugonjwa huo hazina tija.
Shirika la afya duniani, limeonya kuwa maelefu ya visa vingine vya maambukizi huenda vikatokea nchini humo.
Nchi hiyo imeathirika zaidi kutokana na Ebola kuliko taifa lengine lolote kanda ya Afrika Magharibi.
Takriban watu 2,288 wamefariki kutokana na Ebola nchini Liberia, Guinea na Sierra Leone.
Shirika la afya duniani linasema kuwa nusu ya vifo vilivyotokana na Ebola vilitokea wiki tatu zilizopita.
Nchini Nigeria, watu wanane wamefariki kati ya 21 walioambukizwa ugonjwa huo.
Nako nchini Senegal, mtu pekee ambaye alitambulika kuwa na ugonjwa huo ametibiwa na kupona. Hii ni kwa mujibu wa maafisa wa afya nchini humo.
Mgonjwa huyo alikuwa mwanafunzi raia wa Guinea aliyepona kabisa ugonjwa huo baada ya kupokea matibabu.
Bwana Samukai alionya kuwa ugonjwa huo unasambaratisha kila sekta ya nchi hiyo
Mfumo duni wa afya nchini humo,tayari ulikuwa umezidiwa nguvu kuweza kukabiliana na janga la Ebola.
Bwana Samukai aliambia baraza la usalama la Umoaja wa Mataifa kuwa Liberia imekosa uwezo wa kimiundo mbinu na utaalamu pamoja na uwezo wa kifedha kupambana na ugonjwa huo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni