Bondia Pungluang Sor Singyu wa Thailand kushoto akipambana na Fadhili Majiha wa Tanzania wakati wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa Dunia WBO Asia Pacific bantamweight title uliofanyika katika uwanja wa shule ya Amphawa iliyopo Bangkok, Thailand Majiha alipigwa kwa point
Bondia Fadhili Majiha wa Tanzania kushoto akipambana na Pungluang Sor Singyu wa Thailand wakati wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa Dunia WBO Asia Pacific bantamweight title uliofanyika katika uwanja wa shule ya Amphawa iliyopo Bangkok, Thailand Majiha alipigwa kwa point.(P.T)
Na Mwandishi Wetu
BONDIA nambari moja kwa ubora nchini Tanzania katika uzito wabantamweight Fadhili Majiha 'Stoper' mwishoni mwa wiki iliyopita alikuwa na kibarua kizito kutoka kwa Mthailand aliyemenyana nae nyumbani kwao Thailand na kupigwa kwa point.
Akizungumzia matokeo hayo ya kupigwa kwa point bondia huyo amejigamba na kusema kuwa yeye alistaili ushindi hivyo wamempa kwa kuwa kacheza kwao na mcheza kwao utunzwa mana nilicheza kwa ustadi wa ali ya juu na wapenzi wote wa ngumi walikuwa upande wangu wakitafakali kwa nini nilinyimwa ushindi bondia huyo ambaye anatamba sana hapa nchini kuwa hakuna wa kumbabaisha ambapo anadai kukimbiwa mara mbili na bondia Fransic Miyeyusho pamoja na Nassibu Ramadhani ambao wote amewapa onyo ole wake mmoja wao akaingia anga zake atakiona cha moto kwa kuwa mechi zao nyingi wanapenda kupangiana wenyewe kwa wenyewe.
Nimerudi nyumbani nipo fit sina ata kovu la aina yoyote hile hivyo nitahakikisha nafanya mazoezi kuendeleza ufiti niliokuwa nao na napenda kutoa tahadhali kwa bondia yoyote mtanzania atakayejitokeza kwa sasa mbele yangu yeye atakuwa halali yangu.
Nae Kocha wake Waziri Chara amejigamba kwa kusema kuwa bondia wake ni wa kimataifa ambapo michezo yake karibia mitatu kacheza Philippines na mwingine Thailand hivyo wao ni wa kimataifa zaidi mana mapambano aliyocheza nje yote yalikuwa magumu na raundi ni 12 ambapo zote alimaliza kwa kuwa nilimjenga katika mazingira mazuri mabondia wengi wakienda nje ya nchi wengi wao wanapigwa raundi ya kwanza au ya pili au hawafiki ya nne.
Mfanyakazi mmoja wa Liberia katika Shirika la madaktari la Medecins Sans Frontieres (MSF) anaeleza namna alivyopoteza familia yake kubwa kutokana na ugonjwa wa Ebola.
Tayari ametenganishwa na familia yake kutokana na kazi yake, habari hizo zilikuwa ni vigumu kuvumilia kwa namna zilivyomuumiza.
Lakini aliokolewa katika hali ya kuchanganyikiwa baada ya kusikia mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 18 ambaye alikuwa mtu wa 1,000 kutibiwa na taasisi moja ya kujitolea kupona maambukizi ya virusi vya Ebola.
Simulizi ya Alexander Kollie:
Tarehe 21 Septemba, ni siku ambayo sitaweza kuisahau: Nilikuwa nje nikifanya kazi na shirika la MSF kama afisa uenezi wa afya, nikitembelea vijiji na kuwaambia watu juu ya Ebola. Nikapata simu kutoka kwa mke wangu. Nikajibu simu hiyo lakini hakuna mtu aliyeongea.
Alikuwa akiishi katika mji mkuu wa Monrovia, na watoto wetu watatu, wakati mimi nikiwa nafanya kazi Foya, kaskazini mwa Liberia.
Wakati huo Ebola ilikuwa imeingia Liberia kwa hiyo nikajaribu kuzungumza na familia yangu juu ya virusi vya Ebola na kuwaelimisha, lakini mke wangu hakuamini.
Nilimpigia simu mke wangu nikimtaka kuondoka Monrovia na kuwaleta watoto kaskazini, hakusikia, alipinga kuwepo kwa Ebola.
Baadaye usiku huo, kaka yangu alinipigia simu: "Mke wako amekufa."
Nilisema: "Nini?" Alisema: "Bendu amekufa."
Nilidondosha simu; Niliitupa mbali na ikavunjika vipande.
"Hakuwa na dalili yoyote ya kutapika au kuharisha, lakini alionekana kuchoka"
Alexander Kollie
Tulikuwa pamoja kwa miaka 23. Ni yeye peke yake aliyeelewa fika maisha yangu.
Nilihisi kwamba nilipoteza kumbukumbu yangu yote. Macho yangu yalikuwa wazi, lakini sikujua nilikuwa naangalia nini, Sikuwa naona. Baadaye wiki hiyo hiyo, nilipata simu nyingine kutoka Monrovia.
Kaka yangu, ambaye alikuwa akifanya kazi ya uuguzi, alikuwa akimhudumia mke wangu.
Lakini aliambukizwa na alikufa pia.
Halafu watoto wangu wawili wadogo walichukuliwa kwenda kituo cha matibabu mjini Monrovia, lakini mabinti zangu walikuwa wanaumwa na walikufa.
Nilijisikia kukosa zaidi msaada; Nilikuwa nachanganyikiwa; Sikuwa na uelewa wa jambo lolote.
Mtoto wangu mkubwa wa kiume, James Kollie - ambaye pia anajulikana kama Kollie - alikuwa bado Monrovia katika nyumba ambayo familia yetu ilikuwa ikiugulia, japokuwa hakuonyesha dalili za ugonjwa.
Alinipigia simu na kusema: "Kila mtu ameugua, Sijui nini cha kufanya."
Nilimwambia aje huku Foya akae nami.
Wakati kijana wangu alipowasili, watu kijijini hapa hawakutukubali..
Walituambia kuwa familia yetu wote wamekufa na nimwondoe Kollie.
Nilichukizwa na kauli zao. Nilijua hakuwa na dalili zozote na hakuwa kitisho kwao lakini kwa sababu ya unyanyapaa hawakutaka tukae hapo. Ikabidi tuendelee.
Siku ya pili, japo nilibaini kuwa kijana wangu alikuwa amechoka zaidi ya kawaida yake, niliingiwa na woga juu yake.
Alexander Kollie aliweza kumtembelea mtoto wake katika kituo cha kuwatibu wagonjwa wa Ebola. Hakuwa na dalili zozote za Ebola kama kutapika au kuharisha, lakini alionekana kuchoka.
Nilipiga simu ya mawasiliano kuhusu Ebola na MSF walimpeleka katika kituo cha wagonjwa wa Ebola hapa Foya ili kupimwa.
Wakati majibu yalipotoka na kuonya ana maambukizi ya Ebola, ulikuwa usiku wa mateso kwangu. Usiku mzima nilikuwa nalia na kufikiria kile ambacho kingempata mtoto wangu.
"Acha kulia baba… Dada zangu wamekufa, lakini nitapona na nitakufanya uwe na furaha"
James Kollie
Siku iliyofuata, washauri nasaha wa MSF walinituliza. Waliniambia nisubiri. Kubaki na amani. Nilikaa pamoja nao na kuzungumza kirefu.
Niliweza kumwona mwanangu katika kituo cha matibabu kupitia uzio, na nilimwita: "Mwanangu, wewe ni tumaini langu pekee. Jipe moyo. Dawa yoyote watakayokupa, unatakiwa kutumia."
Aliniambia: "Baba, Najua. Nitafanya hivyo. Acha kulia baba… Dada zangu wamekufa, lakini nitapona na nitakufanya mwenye furaha."
Kila siku washauri nasaha walihakikisha wananiona, na walikaa pamoja nami ili niweze kuzungumza.
Baada ya muda fulani mtoto wangu alianza kuimarika. Alikuwa akitembea tembea hapo lakini nilikuwa na wasiwasi nilipoona kuwa macho yake bado ni mekundu.
Halafu kitu chakushangaza kilitokea, kitu ambacho kwa kweli sikuamini mpaka nilipoona.
Nimeona watu wenye Ebola wakianza kuonekana wenye nguvu na halafu siku inayofuata wanatoka.
Kwa hiyo pia nilikuwa nafikiria, huenda mtoto wangu akawa mmoja wa wale watakaotoka siku inayofuata.
'Uso wa tabasamu'
Hatimaye wakati nilipomwona anatoka nje, Nilijawa na furaha sana sana. Nilimwaangalia na aliniambia: "Baba, ni mzima."
Nilimkumbatia. Watu wengi walikuja kumwona akitoka nje. Kila mtu alijawa na furaha alipomwona akitoka.
Halafu MSF waliniambia, huyo ni mgonjwa wa 1,000 katika kituo hicho kunusurika kutokana na ugonjwa wa Ebola.
James Kollie, mwenye umri wa miaka 18, anataka kusoma baiolojia na kuwa daktari.
Hili jambo kubwa, lakini nilikuwa nashangaa, ni watu wangapi tumewapoteza?
Lakini nina furahi sana kumwona Kollie amepona, lakini ni vigumu kutowafikiria wale tuliowapoteza.
Nilipomchukua na kurejea naye nyumbani, kwa kweli alikuwa na uso wenye tabasamu. Nami pia, nilikuwa na tabasamu kubwa usoni pangu.
Niliamua kumfanyia tafrija ndogo.
Tangu wakati huo, tulifanya kila kitu pamoja. Tulilala pamoja, tunakula pamoja na tumekuwa tukizungumza sana.
Nilimwuliza: "Malengo yako ni nini baada ya kuhitimu sekondari?"
Ni mwanafunzi wa darasa la kumi. Aliniambia anataka kusoma baiolojia na kuwa daktari.
Kwa sasa nitajaribu kila njia kutimiza malengo yake na kufanikiwa katika maisha, ili asiumie sana juu ya mateso aliyopata ya kumpoteza mama yake.
Nilimwaambia: "Kwa sasa mimi ni baba yako na mama yako. Nakufanyia yote kwa sasa."
Ana umri wa miaka 18 sasa, kwa hiyo nitamfanya rafiki yangu… kwa sababu ni mtu peke ambaye naweza kuzungumza naye.
Siwezi kupata mke mbadala, lakini naweza kuanza maisha mapya na mtoto wangu
Mwana Diplomasia kutoka Ghana ambaye pia ni Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa (UN) Kofi Annan amesema ugonjwa wa Ebola ni wa ‘maskini’ na sio matajiri. Annan amesema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na kituo cha CNN ambapo amezungumzia sababu kadhaa zinazopelekea mapambano ya dhidi ya Ebola kuchukua muda mrefu huku maelfu ya watu wakipoteza maisha. Katibu Mkuu huyo mstaafu amesema Ebola ni ugonjwa wa maskini kwa kuwa tangu ugundulike ni takribani miaka 40 imepita, ambapo kwa nchi tajiri ingewezekana kufanyika tafiti ambazo zingesaidia kupata ufumbuzi wa tiba ya ugonjwa huo, kitu ambacho nchi maskini za Afrika hazina uwezo wa kuwekeza kwenye tafiti hizo.
Aidha, Annan ameonekana kuvunjwa moyo na jitihada zinazofanywa na mataifa makubwa ikiwemo Marekani kutangaza utaratibu mwisho wa wiki iliyopita wa kuwaweka karantini wauguzi na madaktari waliotoka Afrika Magharibi kwa siku 21, kitu ambacho kinarudisha nyuma ari ya wahudumu hao kujitolea kusaidia wagonjwa kwenye nchi zilizoathirika na Ebola.
Treni imeangusha behewa maeneo ya Vingunguti reli imeharibika vibaya FFU wameshafika eneo la tukio watu wanakula bakora mtindo mmoja hatakiwi MTU eneo hilo kulikuwa na kontena za mohamed
enterprises na Azam. Angalia
CHANZO NI KUKATIKA KWA PINI LOCK AMBAYO IKASABABISHA JANGA HILO.
Mashuhuda wakiwa pamoja na wana usalama wakiangalia ajali hyo
Tanzania ni moja ya nchi zinaoongoza kwa mimba na ndoa za utotoni, kwa mujibu wa ripoti inayotarajiwa kuzinduliwa hii leo jijini Dar es Salaam na Shirika la Haki za Binadamu duniani.
Hata hivyo nchi hiyo imepiga marufuku ndoa hizo, ambapo mtoto wa kike anaruhusiwa kuolewa anapofikisha umri wa miaka kumi na nane.
Mkoa wa Shinyanga ulio kaskazini magharibi mwa Tanzania ndio unaotajwa kuongoza kwa mimba na ndoa za utotoni, ikilinganishwa na mikoa mingine nchini humo.
Takwimu kutoka mashirika mbalimbali ikiwemo UNICEF zinaonyesha kuwa, kwa siku, watoto 16 wanapachikwa mimba za utotoni.
Kwa mujibu wa wataalamu, hali hii imekuwa ikiendelea kwa muda mrefu na kwa asilimia kubwa imezorotesha maendeleo ya mtoto wa kike katika eneo hilo.
Ili kumwokoa mtoto wa kike kutokana na janga hili, kumekuwa na jitihada mbalimbali kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali za kuwaokoa hasa wale ambao tayari wameshatumbukia katika dimbwi hilo.
Shirika lisilo la kiserikali la Agape limeweza kuwaokoa wanafunzi wa kike wapatao mia mbili, wakiwa wamepitia ndoa za utotoni. Wengine tayari wamezalishwa wakiwa na umri chini ya miaka 13. Hivi sasa wanaanza maisha mapya ya kusoma.
Mmoja wa watoto waliokolewa akiwa amejitambulisha kwa jina la Pili Omar, ana miaka 14 na ni mama wa mtoto mmoja. na amekubali kueleza kilichomsibu."Niliolewa kwa sababu wazazi wangu waliniambia sitaendelea kuwa mzigo kwao, hivyo niolewe ili nianzishe mji wangu."anasema Pili.
Wazazi na walezi wa watoto hawa wanalaumiwa kwa kuwalazimisha watoto wao kuingia katika ndoa za utotoni. Licha ya kukithiri kwa ndoa hizo, pia imebainika kwamba asilimia 99 ya ndoa hizo hazidumu. Harieth Kulwa ni mmoja wa waathirika wa ndoa hizi ambaye ndoa yake imevunjika."Nilidhai kuolewa ndio kutatatua matatizo yangu, kumbe nilijiongezea matatizo. Mwanamume aliyenioa kwanza alikuwa mkubwa kwangu, pili alikuwa mlevi…" Anabainisha Harieth.
Hata hivyo, wanaharakati wa haki za binadamu wanaulalamikia mfumo mzima wa kusimamia sheria kwa kutowachukulia hatua kali za kisheria watu wanaobainika kuwasababishia mimba watoto, wakidai kuwa ni kutokana na vitendo vya rushwa vilivyogubika vyombo vya sheria
Roketi ya safari za anga za juu iliyokua ikielekea Kituo cha Kimataifa cha Anga za juu imelipuka wakati ikiruka kutoka jimbo la Virginia nchini Marekani.
Roketi Antares, yenye urefu wa ghorofa 14 ikiwa imetengenezwa na shirika la Orbital Sciences Corp, ililipuka sekunde chache baada ya kuruka katika kituo cha Wallops Flight Facility.
Chanzo cha tatizo la kulipuka kwa roketi hiyo ya mizigo bado hakijafahamika.
Mipango ya kurusha roketi hiyo ya anga za juu Jumatatu, ilicheleweshwa kutoka na boti iliyokuwa karibu na eneo la maji la kurukia roketi hiyo.
Ndege hiyo ilitarajiwa kuwa ya tatu kupewa kandarasi na Shirika la taifa la kusimamia safari za anga za juu la Marekani, NASA.
Roketi hiyo ilitarajiwa kubeba karibu kilo 2,200 za shehena kwa ajili ya wanaanga sita walioko katika Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu.
"Tutajua kilichotokea, tunatumaini hivi karibuni, na tutaendelea vizuri na mipango yetu," amesema Frank Culbertson, makamu-rais mtendaji wa shirika la Orbital Sciences.
"Wote tumeona hili jambo likitokea kabla katika shughuli zetu, na wote tumeona kampuni husika zikiimarika kutokana na tukio kama hili, na tutafanya vivyo hivyo."
Roketi kabla ya kuruka
Hakuna aliyejeruhiwa, amesema Bwana Culbertson, na kundi la wataalam wachunguzi tayari walikuwa wakipitia data kujaribu kubaini chanzo cha ajali hiyo.
Amesema, Jumatano asubuhi, kazi ya upimaji wa mabaki katika eneo la tukio ingeanza.
Uchunguzi hautarukia kwenye hitimisho lakini kundi moja la uchunguzi litajielekeza kuchunguza injini za roketi hiyo AJ-26 zilizotumika kuinyanyua roketi hiyo kutoka eneo la kurukia, anasema Jonathan Amos, mwandishi wa BBC wa masuala ya sayansi.
"Kwa kweli hizi ni injini za Kirusi zilizoboreshwa ambazo kwa asili zilitengenezwa kwa ajili ya roketi za Urusi za kwenda mwezini za N-1.
"Zilitengenezwa kufikia viwango vya kisasa, lakini moja ililipuka wakati wa majaribio ardhini mapema mwaka huu."
Familia ya Bwana Sata wameiambia BBC kuwa Rais wa Zambia, Michael Sata, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 77 katika hospitali ya London alikokuwa akitibiwa ugonjwa ambao haujatajwa.
Kifo chake kimetokea siku chache baada ya Zambia kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa nchi hiyo.
Mwanasiasa huyo mkongwe aliingia madarakani mwezi Septemba 2011 baada ya kuongoza chama chake cha Patriotic Front, na kumshinda Rupiah Banda, ambaye alikuwa rais wakati huo na chama chake cha Movement for Multi-Party Democracy, kikiwa madarakani kwa miaka ishirini.
Michael Chilufya Sata alizaliwa mwaka 1937 katika mji wa Mpika, eneo ambalo lilikuwa wakati huo ni Northern Rhodesia. Alikuwa muumini wa dini ya Kikristo ya madhehebu ya Katoliki, alifanya kazi kama afisa polisi, mfanyakazi wa reli na mwanachama wa chama cha wafanyakazi wakati wa utawala wa kikoloni. Baada ya Zambia kupata uhuru wake, pia aliishi kipindi fulani mjini London, akiwa mfanyakazi wa reli, na kurejea Zambia, akiwa na kampuni ya teksi.
Akiwa mwenye sauti ya mkwaruzo yakiwa ni matokeo ya kuvuta sigara kwa muda mrefu, Bwana Sata aliibuka katika siasa na kupata umaarufu katika miaka ya 1980. Haraka akapata sifa ya kuwa gavana mwenye kuchapa kazi kwa bidii, wakati akiongoza jimbo la Lusaka na mtu wa utekelezaji kwa vitendo.
Lakini pia alijulikana kama mtu wa kutoa amri, mtu asiyeendekeza urafiki na mkali- na wapinzani wake walisema jina alilopewa la bandia la "King Cobra" alikuwa anastahili kuitwa hivyo.
Kwa mara ya kwanza alionekana kama mtu ambaye angetekeleza ahadi za kupambana na rushwa na kupata ufumbuzi wa tatizo la ajira na kuleta ustawi wa jamii. Lakini kipindi chake madarakani kiligubikwa na kuuzima upinzani wa kisiasa na kudorora kwa uchumi. Bwana Sata ni rais wa pili wa Zambia kufariki dunia akiwa madarakani ambapo Rais Mwanawasa naye alifariki dunia akiwa rais.
Wafanyakazi kampuni inayomiliki lori hilo ambayo bado haijafahamika, wakifanya tathmini ya hasara iliyopatikana.
Sehemu ya matairi ilivyobaki. Sehemu ya juu ilivyoungua. Maofisa wa polisi wakijadiliana la kufanya. …Wakielekea eneo la tukio baada ya kufikia muafaka.Askari wakilinda usalama eneo la ajali.Afisa wa polisi akimpa maelekezo askari wa usalama barabarani. Mashuhuda kila mmoja akieleza lake. Madereva wa bodaboda wakiwa wameacha shughuli zao ili kushuhudia tukio hilo.
LORI la mafuta aina ya Scania likiwa limesheheni dizeli likitokea bandarini jijini Dar es Salaam kuelekea mikoani, liligonga tuta katika Barabara ya Morogoro, eneo la Kimara-Baruti, likapoteza mwelekeo na kupinduka kisha kuwaka moto na kuteketea kabisa.
Jeshi la polisi wilayani Ludewa likiondoka eneo la tukio
majirani wakiuangalia mwili wa marehemu Mgimba.
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Merkion Mgimba (Msuruisi) miaka 70 mkazi wa Ludewa Kijijini katika wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe ameuawa kwa kupigwa nondo kichwani usiku wa kuamkia tarehe 28 Oktoba 2014 akiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana.
Akitoa taarifa katika eneo la tukio mke wa marehemu Bi.Theodora Luoga alisema kuwa marehemu alitoka ndani majira ya saa 5 usiku kwa lengo la kujisaidia haja ndogo lakini ghafla alikutana na mtu nje ya nyumba yake na kuanza kupambana naye ndipo alipozidiwa nguvu na kukimbilia ndani akipiga kelele.
JESHI la Polisi mkoani Pwani limefanikiwa kumkamata Michael William maarufu (Michael dada), mkazi wa Kiluvya, wilayani Kisarawe anayetuhumiwa kuhusika na matukio ya ubakaji wa vikongwe mkoani hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani Ulrich Matei alisema jeshi hilo lilikuwa likimsaka mtuhumiwa huyo kwa kipindi kirefu kutokana na kudaiwa kutenda makosa mbalimbali ya ubakaji wa vikongwe na wanawake na kutokomea kusikojulikana.
Alisema, William alitiwa mbaroni juzi baada ya kudaiwa kuhusika katika tukio la wizi wa mifugo lililotokea wiki mbili zilizopita huko Kiluvya.
Pia kamanda Matei alisema, mtuhumiwa huyo anadaiwa kuhusika katika matukio ya ubakaji zaidi ya 10 ambapo kabla ya kufanya vitendo hivyo alikuwa akiwatishia wahusika kwa mapanga.
“Huyu kijana anayejiita Michael dada ni maarufu kwa matukio ya ubakaji na alilisumbua jeshi letu mara kadhaa kwa kunasua mitego aliyowekewa leo tumelazimika kumleta mbele yenu waandishi ili mumuone ni mdogo lakini ametusumbua sana,” alisema.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mwenyeji wake Rais Mhe Truong Tan Sang wa Vietnam wakati wa mapokezi yake rasmi katika Ikulu ya Hanoi katika siku ya kwanza ya ziara yake rasmi ya siku mbili nchini humo Jumatatu Oktoba 27, 2014
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokea shada la maua akishuhudiwa na mwenyeji wake Rais Mhe Truong Tan Sang wa Vietnam wakati wa mapokezi yake rasmi katika Ikulu ya Hanoi katika siku ya kwanza ya ziara yake rasmi ya siku mbili nchini humo Jumatatu Oktoba 27, 2014Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Mhe Truong Tan Sang wakikagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake wakati wa mapokezi yake rasmi katika Ikulu ya Hanoi katika siku ya kwanza ya ziara yake rasmi ya siku mbili nchini humo leo Jumatatu Oktoba 27, 2014Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na vijana baada ya kutembelea kampuni ya mawasiliano ya VIETTEL Jumatatu Oktoba 27, 2014Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam Mheshimiwa Nguyen Phu Trong, katika Makao Makuu ya Kamati Kuu ya Chama hicho tawala cha nchi hiyo Jumatatu Oktoba 27, 2014
STAA wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel, amesema hakuna ukweli wowote wa yeye kutanua na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu nchini Marekani, kwani alikutana naye ukumbini, akiwa amealikwa na blog iitwayo Vijimambo ambayo hutangaza utalii wa Tanzania nchini humo kila mwaka.Alisema wakati wa safari yake hakuelewa lolote kuhusu Waziri Nyalandu na anashangazwa na yanayozungumzwa hivi sasa kwani baada ya kumsalimia walipokutana, hawakuwahi kuonana tena hadi aliporejea, kwani yeye alikuwa amepangiwa kwenye hoteli ambayo pia ndiyo ukumbi wa shughuli hiyo ulipokuwa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza jambo. “Watu wanataka kunijengea uadui na mke wake Faraja Kota ambaye tunaheshimiana sana, mimi nilialikwa kule nikiwa na wasanii wengine, wanamuziki Kassim Mganga na IT na hata malipo ya kazi yangu nililipwa na wao, wanaosema nilitumia hela za wizara sijui wanataka nini, kama wizara iliwapa fedha hao waliotualika mimi sijui,” alisema muigizaji huyo
MSOMI mashuhuri wa masuala ya kisiasa, utamaduni wa Kiafrika na dini ya kiisilamu wa nchini Kenya, Profesa Ali Mazrui ameaga dunia jana akiwa Marekani.
Profesa Mazrui enzi za uhai wake Mazrui alyekuwa anaishi nchini Marekani, amefariki akiwa na umri wa miaka 81 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Taarifa zinadai kuwa Profesa Mazrui atazikwa mjini Mombasa, Pwani ya Kenya alikozaliwa.
Enzi za uhai wake, marehemu alitoa ombi la kutaka kuzikwa Mombasa akisema angependa kuzikwa katika jumba la kihistoria la Fort Jesus.
Kabla ya kifo chake, Marehemu Mazrui alikuwa anafundisha katika Chuo Kikuu cha Binghamton mjini New York, Marekani.
Ili kuliwekea ushahidi suala hilo, Uwazi lina cha kushika mkononi kufuatia wiki iliyopita, wanafunzi wawili wa shule za msingi wilayani Kinondoni ambako Kamanda Wambura anasimamia jeshi lake walipotea na baadaye kuokotwa wakiwa wameuawa.
Wanafunzi hao ambao miili yao iliokotwa, mmoja akiwa amenyofolewa sehemu za siri ni Glory William (7), mwanafunzi wa darasa la kwanza Shule ya Msingi Msingwa na Joshua Nicolas (12) wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Temboni, zote ni wilayani Kinondoni kwa Kamanda Wambura.
Mama mwingine aliyefiwa akilia kwa uchungu.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii siku ya tukio, mama mzazi wa Glory, Faminian Gabriel alisema:
LICHA ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni kupitia kwa kamanda wake, Camillius Wambura kutumia nguvu kubwa kukanusha kwamba, hakuna matukio ya utekaji wa watoto wadogo, hasa wanafunzi, lakini matukio hayo YAPO!! “Jamani wanaposema hakuna utekaji wa watoto huku sisi wazazi tunalia, si sawa! Nakumbuka siku ya jana (Ijumaa) saa kumi jioni mwanangu Glory alirudi toka shule, nilimkumbatia kwa upendo kisha nikamuacha nyumba ya jirani na mfanyakazi wa ndani.
“Mimi niliondoka kwenda kwenye kazi fulani. Niliporudi sikumkuta Glory nyumbani, nilipoulizia nikaambiwa alikuwa na kijana mmoja,” alisema mama huyo.
Waombolezaji wakiubeba mwili wa mmmoja wa watoto waliuwawa.AFIKA KWA MJUMBE
Haikuwa kawaida ya Glory kuwa mbali na nyumbani jambo ambalo lilinitia hofu. Ilibidi nikatoe taarifa kwa mjumbe ambaye tulisaidiana naye kumtafuta lakini bila mafanikio.”
SERIKALI ZA MTAA WAAMBIWA, WASHANGAA
Baadaye pia nilikwenda kutoa taarifa kwenye ofisi za serikali za mtaa lakini mtoto hakuonekana na wao wakashangaa mazingira ya upoteaji wake.
Mmoja wa kati ya Marehemu wa ajali hiyo aliyetambulika kwa jina la Dennis ambaye anatajwa kuwa mfanyakazi ya Exim Bank tawil la Arusha na kwamba katika ajali hiyo alikuwa na baba yake mdogo.
Haya ndiyo mabaki ya gari hilo baada ya ajali.
Picha hii inadaiwa kupigwa muda mfupi kabla ya kuanza safari .