Jumatano, 26 Novemba 2014

MESSI APIGA HAT TRICK NA KUVUNJA REKODI UEFA

Usiku wa mabingwa wa ulaya uliendelea ten jana kwa mara nyingine kwa michezo nane kuchezwa katika viwanja tofauti barani ulaya. 
FC Barcelona ilikuwa ugenini kucheza na timu ya APOEL Nicosia ya Ugiriki.
Mchezo huo uliisha kwa matokeo ya ushindi wa 4-0 – huku Luis Suarez akiifungia Barca goli lake la kwanza katika mashindano hayo. Wakati huo huo Lionel Messi jana usiku alivunja rekodi ya Raul Gonzales Blanco kwa kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo – baada ya kufunga hat trick kwenye mechi hiyo na kutimiza jumla ya magoli 74, akimuacha nyuma Raul mwenye magoli 71 na Christiano Ronaldo 70.

JAJI WAIOBA ANGURUMA MJADALA WA KATIBA

Wananchi wakiwa katika foleni ya kuingia katika ukumbi wa mdahalo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akizungumza katika mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere kuhusu Katiba inayopendekezwa na kufanyika jijini Dar es Salaam.
Mwanaharakati wa mambo ya vijana Humphrey Polepole na aliyekuwa mjumbe wa Tume ya mabadiliko ya katiba akzungumza katika mdahalo huo.

WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI AZINDUA MRADI WA UFUGAJI SAMAKI ZIWA VICTORIA

unnamed1Mgeni Rasmi Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (wa tatu kushoto) pamoja na wageni wengine waliohudhuria Sherehe hizo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Uchumi, Jeshi la Kujenga Taifa Kanali Felix Samilani, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Raphael M. Muhuga, Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhe. John Henjewele, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara, na Mkuu wa Kiteule cha Bulamba Meja David Msakulo.
unnamed2Mgeni Rasmi Waziri wa Maendeleao ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (MB) akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mradi wa Ufugaji wa Samaki ndani ya Ziwa Viktoria Kiteule cha Bulamba kwa kutumia teknolojia mpya ya vizimba (Cages). Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhe.John Henjewele, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael M. Muhuga.unnamed3Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani akipandikiza vifaranga vya samaki ndani ya Ziwa Victoria, mradi unaotekelezwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Wilaya ya Bunda, Kiteule cha Bulamba kwa kutumia teknolojia mpya hapa nchini ya kuzalisha samaki kwenye vizimba.
unnamed4Picha ya vizimba ambavyo ufugaji wa samaki umeanza mara baada ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kuzindua mradi huo na kupandikiza vifaranga vya samaki. Mradi unatekeleza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Wilaya ya Bunda, Kiteule cha Bulamba kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Economic Social Research Foundation (ESRF), Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Ufugaji wa samaki kwa kutumia teknolojia ya vizimba ndani ya Ziwa Victoria, umekuwa ukitekelezwa pia na wenzetu wa Kenya na Uganda ambao wamepiga hatua kubwa .
unnamed6Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP),  Mratibu Mwandamizi wa Mradi Bw. Nehemia Murusuri (wa kwanza kulia) pamoja na Mwakilishi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Mratibu wa Mradi wa Kuondoa Umaskini, Kukuza Uchumi na Utunzaji Endelevu wa Mazingira, Bw. Telesphory Kamugisha (wa pili kulia). Wengine ni baadhi ya wageni waliohudhuria sherehe hizo.unnamed7Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael M. Muhuga akiongea na wananchi wa Kijiji cha Bulamba wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Ufugaji wa samaki katika Ziwa Victoria kwa kutumia teknolojia ya vizimba (Cages) ambayo ni teknolojia mpya ndani ya nchi yetu.unnamed8Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani akitoa hotuba kwa wananchi wa kijiji cha Bulamba (hawapo pichani) mara baada ya kuzindua Mradi wa Ufugaji wa Samaki ndani ya Ziwa Viktoria. Aliwasisitiza wananchi kujiunga katika vikundi ili kujijengea uwezo wa kuanza kutumia teknolojia ya kisasa ya kuzalisha samaki kwa kutumia vizimba (Cages) katika ziwa Victoria.unnamed9Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (mwenye Kaundasuti nyeusi) akionyesha umahiri wake wa kucheza ngoma ya asili mara baada ya uzinduzi wa mradi huo.

Alhamisi, 20 Novemba 2014

APIGWA RISASI NDANI YA GARI LAKE NA KUPORWA BEGI



Mtu asiyefahamika akiwa ndani ya gari lake mara baada ya kupigwa risasi tumboni. Kushoto kwake ni mwanamke aliyekuwa naye garini.
....wapita njiawakijaribu kutoa msaada kwa mtu huyo.…
Mtu asiyefahamika akiwa ndani ya gari lake mara baada ya kupigwa risasi tumboni. Kushoto kwake ni mwanamke aliyekuwa naye garini.
....wapita njiawakijaribu kutoa msaada kwa mtu huyo.
Muonekano wa nyumba wa gari hilo.
...hawa jamaa nao waligongana, mwendesha pikipiki na mwenye gari katika eneo la tukio na kuanza 'kuzikunja'.
Mtu mmoja ambaye hakuweza kujulikana jina lake mara moja amepigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi na kuporwa mkoba uliyokuwa garini ambao haukujulikana ulikuwa na nini ndani yake. Tukio hilo limetokea leo majira ya mchana maeneo ya Magomeni Mikumi jirani na kwa Sheikh Yahaya jijini Dar es Salaam. Mtu huyo alipigwa risasi tumboni akiwa kwenye gari yake Toyota Mark II (GX 100) yenye namba za usajili T487 AZW. Kwenye gari hiyo, alikuwemo mwanamke mmoja akiwa amekaa kwenye kiti cha mbele cha abiria ambaye hakujeruhiwa.
PICHA: HANS MLOLI/GPL

TAREHE YA KUJIANDIKISHA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA HII HAPA


 Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa Bwn. Khalist Luanda akizungumuza na waandishi habari juu ya kukamilika kwa maandalizi ua uchaguzi wa Serikali za Mitaa miji Dodoma leo. Bwn. Khalist Luanda alitangaza rasmi tarehe ya kujiandikisha na kupiga kura.(Picha na habari kutoka Oya Waziri Mkuu TAMISEMI)
Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Bwana Kharist Michael Luanda amesema wananchi wanapaswa kujiandikisha katika daftari maalum la kupigia kura kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuanzia tarehe 23/11/2014 hadi tarehe 29/11/2014. 

WAKAMATWA NA DOLA FEKI TANGA

Dola bandia

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Fresser Kashai akiwaonyesha waandishi wa habari mkoani hapa Dola Feki za kimarekani. Picha na Elizabeth Kilindi, Tanga.
Na Elizabeth Kilindi, TANGA

WATU watatu wanaojishughulisha na biashara ya uuzaji wa noti bandia mkoani Tanga wamekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa wakiwa na dola za kimarekani zenye thamani ya 11200 ambazo ni sawa na shilingi milioni 20 za Kitanzania.

Jumapili, 9 Novemba 2014

AKAMATWA AKIUZA NYAMA YA DOG

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Ahadi Jesikaka Mkazi wa Kijiji cha Ngyekye kwa kosa la kuwauzia watu nyama ya mbwa.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ahmed Msangi amewataja watu waliouziwa na kutumia kitoweo hicho kuwa ni Enock Nsemwa, George Nsemwa, Anyandwile Mbwilo wote wakazi wa Ngyekye

MISS TANZANIA AJIUZULU



Aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu katika pozi na mshindi wa pili, Lillian Kamazima (kulia) aliyechukua nafasi yake pamoja na mshindi wa tatu, Jihhan Dimachk.
Sitti Abas Mtemvu amelivua taji hilo baada ya kuiandikia barua Kamati ya Miss Tanzania, November 5 mwaka huu, kuhusiana na uamuzi wake huo.
Mrembo huyo alikuwa akikabiliwa na shutuma za kudanganya umri wake, jambo ambalo lilililazimu Baraza la Sanaa la Taifa, (Basata) kutokana na agizo la wizara husika kufuatilia ukweli wake.
“Baada ya kutwaa taji la urembo la Miss Tanzania kumezuka shutuma mbalimbali dhidi yangu. Wameniwekea maneno mengi sana mdomoni kwamba nimesema wakati siyo,” amesema kwenye barua hiyo.
“Shutuma hizo zimeandikwa katika vyombo mbalimbali vya habari, blogs na mitandao ya kijamii, kiasi ambacho naweza hata kuhatarisha maisha yangu. Sasa kwa hiari yangu tena bila kushawishiwa na mtu na kwa kulinda heshima yangu na familia yangu natamka rasmi kuvua taji la urembo la Miss Tanzania 2014,” ameongeza.

“Napenda niwashukuru wale wote waliokuwa wakinipa sapoti tangu mwanzo nilipoingia katika mashindano haya katika ngazi ya taifa, na warembo wote wa Chang’ombe, Temeke pamoja na wote tuliokuwa nao katika fainali za Taifa. Pia napenda kutuma shukrani za dhati kwa waandaji wote wa kituo cha Chang’ombe, Temeke na wajumbe wa Kamati ya Miss Tanzania kwa mafunzo mbalimbali niliyopata. Nawashukuru pia waandishi wote kwa mchango wenu, pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo na Baraza la Sanaa kwa busara zenu.”
Aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu katika pozi.
“Leo nalivua taji rasmi nililopewa na binadamu lakini alilonipa mwenyezi Mungu bado ninalo. Mwisho naomba radhi Watanzania wote kwa uamuzi huo niliochukua.” Nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa mshindi wa pili, Lilian Kamazima.

HELIKOPTA YA MCHUNGAJI GWAJINA YAZINDULIWA

Rubani wa helikopta hiyo akijiandaa kuirusha helikopta hiyo.
Helikopta ikiwa hewani.
Hapa ikijiandaa kutua.

Helikopta ya Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima imezinduliwa leo hii katika viwanja vya Tanganyika Packers, vilivyopo Kawe jijini Dar na kuhudhuriwa na maaskofu wa makanisa mbalimbali wa madhehebu ya Kikristo nchini.
Uzinduzi huo pia uliohudhuriwa na Mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowassa ambaye alikuwa mgeni rasmi wa uzinduzi huo ulioendana na kukata utepe kisha kuirusha helikopta hiyo hewani kama ishara ya kuanza rasmi kazi yake ambayo ni kutoa msaada wa usafiri wa haraka wakati wa dharura na kuhubiri injili kupitia helikopta hiyo.

Jumatatu, 3 Novemba 2014

KINYWAJI CHA SHUDA COCKTAIL CHAZINDULIWA DAR

Kampuni ya A&K HOLDINGS LTD mwishoni mwa wiki iliyopita ilizinduz kinyaji cha Shuda Cocktails hafla iliyofanyika Novemba 1, 2014 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, kinywaji hicho kimetengenezwa kwa ufanisi na kuchanganywa katika vipimo maalum ili kupata bidhaa zenye ladha nzuri zinazolenga na kukubalika na matabaka yote ya wanywaji au watuamiaji wa vileo. Ujazo wake ni 700ml. Bidhaa hii inazalishwa nchini Uingereza.
Meneja Masoko ya Kinywaji cha Shuda Cocktails, Bernadetha Daudi akiongea katika uzinduzi wa kinywaji huo mwishoni mwa wiki iliyopita Nobemba 1, 2014 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya A&K HOLDINGS LTD ambao ni wasambazaji wa kinywaji cha Shuda Cocktails akiongea katika uzinduzi wa kinywaji hicho, halfa iliyofanyika  mwishoni mwa wiki iliyopita Novemba 1, 2014 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Shuda Cocktails zipo katika ladha nne kwa sasa: Woo Woo, Pina Colada, Mojito na On the Beach. bei ya rejareja ni Tsh 12,000 kwa chupa.
Mabinti waliokipamba kinywaji cha Shuda Cocktails.
Balozi wa Kinywaji hicho, Lemtuz akiwa na mabinti wakikipamba kinywaji cha Shuda Cocktails.

Kwa sasa zinapatikana katika supermarket zote hapa Dar es salaam, kumbi za starehe na bar kwenye kila kiunga cha Dar es salaam. Hivi karibuni, Shuda Cocktails zitapatikana mikoani pia.
Ofisi zetu zipo Masaki, Kahama Rd mkabala na Mafian Lounge ya zamani.

Ili kupata maelezo zaidi kuhusiana na shuda Cocktails tembelea tovuti yetu www.shudacocktails.tz.co na facebook kupitia Shuda Cocktails Tanzania
Tunapatikana pia kupitia namba +255 717923963 na 0717 528216.

Kila aina ya Shuda ina viungo tofauti kama ifuatavyo:
Shuda Woo Woo; Cranberry juice, peach schnapps and Vodka
Shuda PinaColada: Pineapple juice, banana, Coconut milk and rum
Shuda On the Beach: Peach schnapps, orange juice, vodka
Shuda Mojito; Lime juice, club soda, mint and rum

BENKI YA IWEKEZAJI ULAYA YAIPA MKOPO CRDB

BENKI ya CRDB imesaini mkataba wa mkopo wa sh. bilioni
43 baina ya benki ya uwekezaji Ulaya (E.I.B)
kwa ajili ya kuwakopesha na kuwasaidia wafanyabiashara wanaofanya shughuli za
kukuza uchumi.
 
Akizungumza jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki Mkurugenzi Mtendaji
wa CRDB, Dk. Charles Kimei alisema benki yake kwa kushirikiana na EIB imeamuwa
kusaidia jamii nchini hivyo mkataba huo ni mwanzo wa ushirikiano endelevu
utakaohamasisha upatikanaji wa ajira.
 
Alisema kufanyakazi na benki ya EIB kutasaidia kukuza
biashara katika maeneo muhimu kama uvuvi, usindikaji wa chakula, usafiri,
biashara pamoja na huduma zote za kiuchumi.
 
“Mimi kama kiongozi wa CRDB Tanzania ninamamlaka ya
kusaidia hizi sehemu za soko na kuongeza jitihada za kumaliza umaskini, pia
kuongeza shughuli za kiuchumi za wateja wetu ili kufikia lengo la kuongeza
mapato katika benki yetu,” alisema Kimei.
 Kwa upande wake Naibu
Waziri wa Fedha Adam Malima alisema mkataba huo pia una lengo la kuisaidia
benki ya CRDB katika kuendesha shughuli zake mbalimbali.
 
Alisema ni jambo la faraja kuona benki kama EIB imekubali
kuiamini CRDB na kuipa mkopo wa kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya kuwasaidia wafanyabiashara.
“Tunachokiamini kuwa hii benki kutoka Ulaya siyo benki
ndogo ni kati ya benki kubwa zilizopo hapa duniani, sasa kama wamekuja hapa
kwetu na wakaonyesha nia njema ya kutusaidia endapo watabaini kuwa pesa zao azitatumika
kwa malengo yaliyokusudiwa watavunjika moyo,” alisema
 
Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima akiwasili ukumbini wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba wa mkopo wa sh. Bilioni 43 kutoka Benki ya Uwekezaji Ulaya. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi CRDB, Martin Mmari na (katikati) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei na kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa.Mwakilishi wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya, Nikolaos
Milianitis (kulia) akisaini mkataba wa mkopo wa sh. bilioni 43 na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB,
Dk. Charles Kimei baada ya Benki hiyo kwa ajili ya kuwakopesha wafanyabiashara Wadogo na Wakati. Hafla hiyo
ilifanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Wa pili kushoto anayeshuhudia ni Naibu Waziri wa
Fedha, Adam Malima. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari na Wa pili kulia ni, Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya, Eric Beaume.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA UTOAJI WA KIFAA KWA WALEMAVU WA USIKIVU

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akizindua rasmi utoaji wa huduma kwa walemavu wa kusikia (Viziwi) uzinduzi huo umefanyika leo Novemba 3, 2014 kwenye Viwanja vya Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, chini ya usimamizi wa Taasisi ya Starkey Hearing ya nchini Marekani.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, Mwasisi na Rais wa Taasisi ya Hearing, William Austine, baada ya uzinduzi wa huduma kwa walemavu wa kusikia (Viziwi) uzinduzi huo umefanyika leo Novemba 3, 2014 kwenye Viwanja vya Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, chini ya usimamizi wa Taasisi ya Starkey Hearing ya nchini Marekani.

JAJI WARIOBA AONJA JOTO YA JIWE KATIKA MDAHALO WA KATIBA MPYA

Jaji Joseph Warioba akitoa mada. 
Mtoa mada katika mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa, Jaji Joseph Warioba akitoa mada kabla ya mkutano huo kuvunjika katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Saam.
Baadhi ya vijana walioingia na mabango ndani ya ukumbi wa mkutano wakiwa na mabango yaliyokuwa yakisomeka ‘Katiba inayopendekezwa tumeipokea tunaiunga mkono’.
Mlinzi wa Jaji Joseph Warioba (kushoto) akimkinga kwa mikono ili asipate madhara baada ya mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa kuvamiwa na kundi la vijana na kusababisha uvunjifu wa amani. 
Jaji Joseph Warioba akiangalia usalama wake kabla ya kuondolewa mlinzi wake katika ukumbi wa Ubungo Plaza ambapo mdahalo wa kuijadili Katiba inayopendekezwa ulikuwa ukifanyika kabla ya kuvunjika.
Aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole akimzuia mmoja wa vijana aliyekuwa na jazba mara baada ya kutokea kwa vurugu katika mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekeza.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Joseph Butiku (katikati) akisindikizwa kuingia katika chumba cha VIP mara baada ya kuvunjika kwa mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa. Mdahalo huo uliandalia na taasisi hiyo.
 Vijana wakiwa na mabango. 
 Mabango yakiwa juu. 
 Vujo zinaanza. 
 Mmoja wa vijana waliokuwa wakitoa maneno ya kashfa kwa Jaji Warioba akiwanyooshea vidole viongozi wa meza Kuu. 
 Baadhi ya viti vilivyovujwa. 
 Jaji Warioba akitoka katika ukumbi huku akisindikizwa na askari kanzu. 
 Jaji Warioba akisindikizwa na makachero wa Polisi. 
 Jaji Warioba akiwapungia mkono wananchi waliokuwa wamefurika nje ya jengo la Ubungo Plaza ambako mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa ulikuwa ukifanyika.Wananchi waliokuwa nje ya jengo la Ubungo Plaza wakimshangilia Jaji Warioba wakati akitoka katika ukumbi wa mdahalo huku wakimuita 'Rais Rais'.(Picha zote na Francis Dande).