Watu
wawili wamenusurika kifo baada ya dereva wa bodaboda kumgonga mtu mmoja
aliyekuwa akivuka katika barabara ya Kawawa Kinondoni na kisha dereva wa
boda boda kukimbia kusikojulikana huku abiria wake pamoja na mvuka
barabara huyo wakiwa katika hali mbaya.
Tahadhari juu ya
uendeshaji salama vyombo vya moto barabarani umeendelea kupigiwa kelele
kila uchao haswa katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka lakini bado
inaonekana kama hadithi za sungura na fisi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni