Hii leo kulikuwa na taharuki katikati mwa jiji la Nairobi
baada ya Punda waliokuwa wamepakwa rangi kupatikana wakizurura mjini humo.
Walikuwa na maandiko katika mwili wao yakisema: 'Tumechoka'
Neno 'Tumechoka' ni kauli mbiu ambayo ilitumiwa na mashirika
ya kijamii kuelezea wasiwasi kuhusu hali ya utovu wa usalama nchini kote.
Baadhi ya wananchi walishangaa Punda walikuwa wanafanya nini
mjini kumbe wanaharakati ndio waliowaleta huko kuonyesha kuchoshwa kwao na kuzorota kwa usalama nchini humo.
Kauli
mbiu hio ilitumiwa mashambulizi yalipofanywa dhidi ya wakenya mjini
Mandera Kaskazini mwa Kenya ambapo wanaharakati walipiga kambi katika
ofisi ya Rais wiki kadhaa zilizopita kulalamikia ukosefu wa usalama.
Kwa kutumia Punda, kupitisha ujumbe wao, ni dhahiri kuwa ujumbe wao umefika kwa wengi.
Wanaharakati hao, wamewahi kutumia Nguruwe kuonyesha walivyo walafi na wafisadi wanasiasa wa Kenya.
Punda hao
walikuwa 22 na walifikishwa kati kati ya mji kwa Lori. Dereva wa lori
hilo alisema kuwa alilipwa na mtu fulani kupeleka wanyama hao mjini.
Lori hilo lilipofikishwa mjini, mwanamume aliyekuwa amekodisha lori hilo aliamua kutoka kwenye Lori na wanyama hao.
Polisi wamesema wanachunguza kujua nani waliofanya kazi hiyo.
Wanyama hao walinuiwa kutuma ujumbe kwamba wakenya
wamechoshwa na hali mbaya ya usalama, alisema mwanaharakti mmoja aliyekuwa
kwenye Lori hilo.
''Tumechoshwa na uongozi mbaya, '' alisikika akisema
mwanaharakati mmoja huku akiwasukuma Punda hao kutoka kwenye Lori.
Polisi wanasema wanawasaka wale waliohusika na kitendo
hicho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni