Waziri mkuu wa zamani mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa na mkewe
mama Regina Lowassa wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu mzee
Lazaro ole Ngoilenya Laizer aliyefariki juzi na kuzikwa jana Alhamis
kijijini kwake Ngarash Monduli.Mzee Ole Ngoilenya ambaye amefariki akiwa
na umri wa miaka 120 alikuwa muasisi na kiongozi wa kwanza wa Chama Cha
TAA na baadaye TANU wilayani Monduli wakati huo ikijulikana kama Maasai
District. Pia ndiye alikuwa chachu kwa Mh Lowassa na wanasiasa wengine
wa Monduli kuingia katika siasa. Alioa wake 9 na kufanikiwa kupata
watoto 53.
Waziri mkuu wa zamani mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa na mkewe
mama Regina Lowassa wakitoa pole kwa wafiwa baada ya kutoa heshima za
mwisho kwa mwili wa marehemu mzee Lazaro ole Ngoilenya Laizer
aliyefariki Jumanne na kuzikwa Alhamisi kijijini kwake Ngarash Monduli.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni