Utandawazi unatajwa kuwa kiunganishi muhimu cha maisha ya kisasa
kinachoubadilisha uchumi wa nchi kuwa wa kimataifa, lakini unalaumiwa
pia kwa kutoweka kwa UĂștambulisho wa tamaduni asilia.
Utandawazi unaufanya ulimwengu kuwa kijiji lakini kwa gharama za kuupoteza utambulisho wa tamaduni asilia.
Vijana wengi wa sasa wanakuwa na kuishi huku wakiimarisha dunia nzima na
kujieleza wenyewe kuwa ni watu wasiomilikiwa na utamaduni wowote. Mwaka
2013, watu milioni 232, au asilimia 3.2 ya idadi ya watu duniani,
walikuwa wahamiaji kwa mujibu wa sheria za kimataifa, ikilinganishwa na
watu 175 milioni mwaka 2000 na 154 milioni mwaka 1990.Matokeo ya takwimu hizo ni idadi kubwa ya watu ulimwenguni kuoana kutoka watu wa tamaduni mbalimbali, dini na makabila. Kwa mfano wa Barani Ulaya katika kipindi cha mwaka 2008 hadi mwaka 2010 kwa wastani wa mtu mmoja kati ya watu 12 waliofunga ndoa, ndoa yake imechanganyika na watoto wao wanakuwa katika uzazi wa mchanganyiko na wakati mwingine ni wenyeji wa nchi waliomo kama wazazi wote ni wahamiaji.
Mwaka 2013, zaidi ya watu bilioni moja walisafiri kimataifa kama watalii, na kuongeza ujuzi wao wa kwanza duniani wakiwa nje ya mipaka ya wanamoishi. Kwa upande mwingine, kuna karibu watu bilioni tatu wanatumia huduma za kimtandao yani Internet katika dunia ya leohuku kukiwa na zaidi ya watu bilioni waliojikita katika matumizi ya mitandao ya kijamii katika sayari ya dunia.
Utandawazi kama utamaduni maalum
Utamaduni na utandawazi umeanza kueleweka kama upande pekee utamaduni maalumu huku kukiashiria kuwa na mkusanyiko wa utamaduni wa aina moja.
Uelewa binafsi kwa raia ulimwenguni na utambulisho wa utamaduni unaelezwa na ukosefu wa kuwa na umiliki wa utamaduni maalumu.
Wananchi ulimwenguni wamepoteza hisia zao za umiliki wa asili na kuwa wageni katika jamii lakini wanapatiwa uhuru wa kujieleza wenyewe na kujitegemea pindi wanapokuwa huru bila ya kuwepo kwa vikwazo kutoka kwa jamii au utamaduni.
Ulimwengu mpya wa utamaduni ni kujitokeza kwa njia ya maono muhimu, ambayo ni huru kwa mila zilizopo na maadili yenye hifadhi ikiwa ni kwa kuanzisha njia mpya ya kufikiri katika suala la ujumla lisilogawanyika, na kusahaulika kwa uwiano wa maadili kulinganishwa na utambuzi wa thamani halisi ya kila kitu na kila mtu.
Maendeleo ya kisasa na kupotea kwa utamaduni
Harakati za kiraia ulimwenguni zinatakiwa kuungana na nia za watu ili kuendeleza amani na ulimwengu endelevu ili kuharakisha mshikamano na harakati za kimataifa katika mabadiliko binafsi na ya kijamii ili kuonyesha umoja wenye ubinadamu.
Kuongeza idadi ya watu, jamii, hata makampuni ya ushirika kuzinazidi kueleweka na kuwa muungano wenye faida ya ushirikiano kama mtindo wa biashara.
Wananchi wa kweli ulimwenguni wana lengo la kuunganishwa katika jamii,makundi, na watu binafsi katika ngazi ya ulimwengu ili kuhamasisha uelewa wa ubinadamu wenye kuzingatia kitu kimoja na kuongeza namna ya kujieleza kupitia amani, usawa wakijamii na usawa wa elimu ya uhusiano wa viumbe na mazingira.
Kuna matatizo ya kimfumo, hivyo kuna hitajika utaratibu ilikupata ufumbuzi ambao ni nguvu moja pekee duniani ya kutosha kutatua tatizo hili kwa umoja wa watu wote.
Kuibuka kwa tahadhari kulikojitokeza kila mahali kumewafanya watu kuwa na ufahamu katika nyanja nyingi za taasisi za kisiasa ambapo mfumo wa maisha kiutendaji upo chini ya kiwango na ustawi wa maisha ya binadamu upo katika hatari.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni