Jumamosi, 14 Februari 2015

RAIS AFUNGUA KITEGA UCHUMI MOSHI

KJ1Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua jengo la upasuaji katika hospitali ya rufaa ya Mawenzi mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro muda mfupi baada ya kulifungua jana. Kulia ni Naibu Waziri wa Afya Dkt.Steven Kebwe.KJ2Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wauguzi wa hospitali ya rufaa ya Mawenzi mjini Moshi muda mfupi baada ya kufungua jengo la upasuaji na kuweka jiwe la msingi kuzindua ujenzi wa wodi ya kinamama na watoto katika hospitali hiyo jana. (wa nne kulia ni Naibu Waziri wa Afya Dkt.Steven Kebwe, wa nne kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama,Kushoto ni Mbunge wa Vunjo Agustino Lyatonga Mrema,na wa pili kushoto ni Mbunge wa Moshi Vijijini Dkt.Cyril Chami.
KJ3KJ4Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri wa Kazi na ajira Mh.Gaudensia Kabaka (watano kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt.Ramadhani Dau (wa pili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama (wa pili kushoto) pamoja na viongozi na wadau wengine wakikata utepe kufungua rasmi jengo la kitega uchumi la NSSF Kilimanjaro Commercial Complex mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro jana.KJ5Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt.Ramadhan Dau pamoja na wadau wengine wakitazama ramani ya jengo jipya la kitega uchumi la NSSF mjini Moshi Kilimanjaro Commercial Complex wakati wa hafla ya ufunguzi jana.KJ6Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na chipukizi wa Tanzania Girl Guides wakati wa hafla ya ufunguzi wa jengo la kitega uchumi la NSSF mjini Moshi jana. Tanzania Girl Guides, UMATI, Tanzania Red Cross ni wadau wa NSSF katika mradi huo.KJ7Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt.Ramadhani Dau baada ya hafla ya ufunguzi wa jengo jipya la kitega uchumi la NSSF mjini Moshi jana. Katikati ni Waziri wa Kazi na Ajira Mh. Gaudensia Kabaka (picha na Freddy Maro)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni