makundi mbalimbali ya kijamii ya mikoa ya Kaskazini, inayojumuisha mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Manyara wakiwa wanaandamana kwa pamoja kuelekea kwa mbunge wa jimbo la monduli hii leo
Katibu wa
Chama cha Wasioona Mkoa wa Kilimanjaro (TLB), Protas Soka Akisoma
risala kwa niaba ya makundi hayo mbele ya mbunge wa jimbo la Monduli
Viongozi mbalimbali wa makundi ya kijamii wakiwa wanamkabidhi waziri
mstaafu ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Monduli Edward Lowasa bahasha
yenye fedha taslimu shilingi milioni mbili laki tano sitini na saba elfu
na mia sita zilizochagwa na wananchi kwa ajili ya kwenda kuchukuwa
fomu ya kugombea nafasi ya Urais
mbunge wa
jimbo la Monduli akiangalia picha ambayo ametengenezewa na vijana
kutoka makundi wakati walipomtembelea nyumbani kwake monduli kwa ajili
ya kumkabidhi fedha kidogo kwa ajili ya kuchukuwa fomu ya kugombea urais
makundi
mbalimbali ya kijamii ya mikoa ya Kaskazini, inayojumuisha mikoa ya
Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Manyara wakiwa wanaandamana kwa pamoja
kuelekea kwa mbunge wa jimbo la Monduli
makundi
mbalimbali ya kijamii ya mikoa ya Kaskazini, inayojumuisha mikoa ya
Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Manyara wakiwa wanaandamana kwa pamoja
kuelekea kwa mbunge wa jimbo la Monduli
Mratibu
wa Marafiki wa Lowasa Kanda ya Kaskazini, Noel Nnko, akiwa anamuonyesha
picha ambayo ni ya kumbukumbu ya tukio la leo la kuja kumuunga mkono
mbunge wa jimbo la monduli pamoja na kumuomba atangaze nia ya kugombea
nafasi ya urais
maandamano ya pikipiki yakiwa yanaelekea nyumbani kwa mbunge wa jimbo la monduli hii leo
Na Woinde Shizza, Monduli
Wananachi
zaidi ya 700 kutoka makundi mbalimbali ya kijamii ya mikoa ya
Kaskazini, inayojumuisha mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Manyara,
wamejitokeza nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli
(CCM), Edward Lowasa, wakimshawishi atangaze nia ya kugombea urais
kupitia chama hicho.
Wananchi
hao kutoka katika Makundi mbalimbali katika ya mikoa hiyo yamewasili
leo nyumbani kwake,Kijiji cha Ngarashi, Wilaya ya Monduli baada ya
kufanya maandamano makubwa yaliyoanzia njia panda ya Monduli, wakiimba
nyimbo za matumaini kwamba 'wewe ni tumaini la walio wengi Tanzania,
maamuzi na matumaini mapya, watanzania wako nyuma yako'.
Aidha akisoma risala kwa niaba ya makundi
hayo baada ya kuwasili nyumbani hapo , Katibu wa Chama cha Wasioona
Mkoa wa Kilimanjaro (TLB), Protas Soka alisema kwa nia thabiti isiyo na
kigugumizi asilani, wanaharakati hao pamoja na watanzania wengine
wanamhitaji (Lowasa) kwa unyenyekevu na hivyo, wanamwomba atangaze nia
ya kuingia kwenye kinyang'anyiro cha Urais mwaka 2015.
"Leo
watanzania tumepaza sauti zetu kwa pamoja kuanzia ngazi ya
Kaya, Kitongoji, Kijiji, Kata, Tarafa, Wilaya, Kanda mpaka Taifa wakisema
Viva Lowasa, Tobiko Lowasa. Kwa moyo mmoja bila kushawishiwa na mtu wala
kikundi chochote; wanaharakati hawa wamekuona wewe, mheshimiwa Edward
Lowasa ndio kiongozi sahihi kwa mustakabali na manufaa ya taifa
letu,"alisema Soka
Makundi
hayo ambayo ni walemavu, waendesha bodaboda, walimu, wataalam wa afya,
vijana na wanasiasa, walimchangia Lowasa kiasi cha shilingi milioni
2,567,600 kwa ajili ya kununua au kulipia fomu ya kugombea nafasi ya
Urais pindi atakapotangaza nia.
"Kwa
lugha nyingine sasa tunakuomba Mheshimiwa Lowasa
utangaze nia ya kuingia kwenye kinyang'anyiro cha Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,"alisema Soka.
Makundi
hayo yaliyoongozwa na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kilimanjaro, Paul Matemu, Mratibu wa Marafiki wa
Lowasa Kanda ya Kaskazini, Noel Nnko, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa na
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM), mkoa wa Arusha,
Robnson Meitinyiku, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa, Fred Mushi, Askofu
wa Kanisa la Calvary Assemblies of God, Christoher Madilu ambaye pia ni
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa na Abdalah Sadick kutoka mkoa wa
Manyara.
Akizungumza
mara baada ya kupokea makundi hayo mbunge huyo wa jimbo la
Monduli
alisema kuwa amekubaliana nao na anatarajia kutangaza rasmi nia mwezi
Aprili pindi tu chama chake kitakaporuhusu
"Nitatangaza
nia mwezi Aprili mwaka huu, pale uwanja wa Shekhe Amri Abeid mjini
Arusha baada ya chama changu kupuliza kipenga. Ninachowaomba watanzania
kwa sasa, mniombee katika safari yangu ya matumaini,"alisema Lowasa.