Jumanne, 3 Machi 2015

Mpinzani wa Urusi aliyeuwawa azikwa

Waombolezaji nchini Urusi wamejitokeza nje ya kituo cha haki za binadamu mjini Moscwo kwa ajili ya kuhudhuria maziko ya kiongozi wa upinzani aliyeuwawa Boris Nemtsov.
Warusi wauaga mwili wa kiongozi wa Upinzani aliyeuwawa na serikali,Nemtsov Boris Warusi wauaga mwili wa kiongozi wa Upinzani aliyeuwawa na serikali,Nemtsov Boris
Kiongozi huyo wa upinzani aliuwawa kwa kupigwa risasi ijumaa jioni wakati akitembea kwenye daraja la karibu na ikulu ya Kremlin akiwa pamoja na mpenzi wake. Hadi sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.
Mwili wa marehemu Nemtov umelazwa kwenye sanduku ukiwa umevishwa sanda nyeupe katika kituo cha haki za binadamu cha Sakharov mjini Moscow, kituo ambacho kimepewa jina la aliyekuwa mpinzani enzi za utawala wa kisovieti na aliyewahisi kutunukiwa tuzo ya amani ya Nobel Andrei Sakharov. Mauaji ya kiongozi wa upinzani wa Urusi Boris Nemtsov yameitikisa kwa kiasi kikubwa jamii ya vuguvugu dogo öla upinzani na ambalo limetengwa nchini Urusi.
Misururu ya waombolezaji waliojitokeza katika mazikoni,Moscow 
  Misururu ya waombolezaji waliojitokeza katika mazikoni, Moscow
Wengi wa wafuasi wa upinzani nchini humo wanashuku mauaji hayo yamefanywa kwa amri ya serikali ya Urusi kama hatua ya kulipiza kisasi kauli za mpinzani huyo za kumkosoa rais Vladmir Putin. Maafisa wa Urusi wameashiria kwamba kuna uwezekano mkubwa wa sababu zamauaji hayo kuwa zimetoakana pia na uchokozi ulioonekana kulenga kumchafua rais Putin. Nemtsov anazikwa leo mjini Moscow wakati ambapo baadhi ya wabunge maarufu kutoka Ulaya wamearifu kwamba wamezuiwa na nchi hiyo ya Urusi kuhudhuria maziko hayo.
Mabalozi wengi wa nchi za magharibi walitarajiwa kuhudhuria shughuli ya maziko iliyoanza asubuhi ya leo kwenye kituo cha Sakharov kabla ya maiti kuzikwa mchana wa leo kwenye makaburi yaliyoko nje ya eneo hilo. Hadi sasa kuna wawili mashuhuri kutoka Ulaya waliosema wamezuiwa na Urusi kuhudhuria maziko hayo.
Wafuasi wa upinzani wamejitokeza kwa wingi kumzika Nemstov akiwemo Mama yake mzazi Wafuasi wa upinzani wamejitokeza kwa wingi kumzika Nemstov akiwemo Mama yake mzazi
Aliyekuwa waziri wa nje wa Latvia Sandra Kalniete ambaye ni mbunge katika bunge la ulaya amesema lizuiwa na walinzi kuingia kwenye uwanja wa ndege wa Sheremetyevo mjini Moscow jana usiku.Mbunge huyo ametoa taarifa baada ya kuzuiwa uwanja wa ndege akisema licha ya uamuzi huo wa serikali ya Putin anataka kuifahamisha familia ya Nemtsov pamoja na marafiki zake na wananchi wote wa Urusi wanaounga mkono Demokrasia watambue kwamba Ulaya ipo pamoja nao wakati huu wa majonzi.
Mwingine aliyezuiliwa na Urusi kuhudhuria maziko hayo ni rais wa baraza la seneti la Poland Bogdan Borusewicz aliyesema kwamba amenyimwa visa ya kuingia nchini humo.Shahidi mkuu wa tukio la mauaji ya Nemtsov ni mpenzi wake aliyekuwa naye wakati huo wa tukio Anna Duritsskaya ambaye anaendelea kushirikiana na kamati ya uchnguzi.Hata hivyo bibi huyo amerudi nyumbani kwao Ukraine.
Mwandishi:Saumu Mwasimba

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni