Mmoja wa wanaharakati wakuu wa kupigania haki za kikatiba nchini Msumbiji ameuawa kwa kupigwa risasi katika mji mkuu wa Maputo.
Gilles
Cistac, ambaye anaasili ya Ufaransa amehusika pakubwa katika mchakato
wa kugawanya madaraka katika serikali ya majimbo na ugavi wa mamlaka
nchini Msumbiji.Cistac alikuwa anapigania sera hiyo iingizwe katika katiba ya taifa jambo ambalo lilimfanya kutizamwa kama mtu anayependelea chama cha upinzani Renamo.
Afisa mkuu wa Afya katika hospitali kuu ya Maputo Joao Fumane amesema Cistac alipoteza maisha yake muda mchache baada ya kufanyiwa upasuaji.
'Mtu maarufu'
Awali msemaji wa rais Filipe Nyusi alikashifu mauaji hayo akisema kuwa hiyo ilikuwa tukio la kukera zaidi.
Mwanaharakati huyo ambaye pia ni mkufunzi katika chuo kikuu kitivo cha sheria alichangia kwa kina mchakato wa kubadilisha vipengele vya mamlaka ya urais.
Cistac alikuwa amepata uraia wa taifa hilo baada ya kuishi huko kwa tangu mwaka wa 1993.
Aidha mbali na kufundisha katika chuo kikuu cha Eduardo Mondlane, alikuwa amehudumu kwa kipindi kirefu kama mshauri wa maswala ya sheria katika wizara mbalimbali.
Katika miaka ya hivi punde kulikuwa na shauku ya kuzuka upya vita vya wenyewe kwa wenyewe baada ya kundi la Renamo, kulalamika kuwa uchaguzi uliofanywa nchini humo haukuwa wa haki.
Renamo ilisitisha mapigano mwaka wa 1992 baada ya kukabiliana na serikali kwa kipindi cha miaka 16.
Kiongozi wake Afonso Dhlakama alikubalia mwito wa kujaribu kutafuta uwiano kupitia kwa bunge la taifa.
Inaaminika kuwa rais Filipe Nyusi, ndiye aliyewashawishi wabunge wa Renamo kujiunga na serikali .
Chama hicho kilichojizolea asilimia 36% ya kura za urais zilizopigwa mwezi Oktoba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni