Makao makuu ya kanisa katoliki duniani Vatican yanasema kuwa nguvu
inaweza kutumiwa kusitisha mashambulizi yanayoendeshwa na wanamgambo wa
Islamic State dhidi ya wakristo na makundi mengine madogo .
Askofu
mkuu Silvano Tomasi ambaye ni mwakilishi mkuu wa Vatican kwenye umoja
wa mataifa mjini Geneva ameyashutumu makundi ya jihad kwa kuendesha
mauaji ya halaiki.Akizungumza kupitia mtandao wa Vatican amesema kuwa hatua za kijeshi zitaanzishwa ikiwa suluhu ya kisiasa haitapatikana.
Lakini amesema kuwa muungano wowote dhidi ya Islamic State ni lazima ujumuishe nchi za kiislamu kutoka mashariki ya kati.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni