Kocha
wa Arsenal Arsene Wenger anaamini kuwa kilabu hiyo bado ina fursa ya
kuibandua Monaco katika michuano ya kilabu bingwa barani Ulaya licha ya
kucharazwa 3-1 katika awamu ya kwanza ya mechi hizo.
Arsenal
itakabiliana na timu hiyo ya Ligi ya daraja la kwanza siku ya jumapili
huku ikiwa hakuna timu ilioweza kufanikiwa kubadilisha matokeo kama hayo
katika michuano hiyo.Wenger:Tuna changamoto kubwa mbele yetu lakini tutafanya kila kitu kuhakikisha kwamba tunafuzu kwa robo fainali.
''Wao ndio wanaopigiwa upato kufuzu lakini tunaweza kubadilisha mambo''.
''Tutahakikisha kuwa tuna hamu na imani ya kushinda''.
Arsenal italazimika kufunga bao tatu kwa bila ili kuweza kufuzu kwa robo fainali.
Tayari kilabu hiyo imepata motisha kufuatia ushindi wao wa mabao 3-0 dhidi ya kilabu ya West Ham siku ya jumamosi. .
Tayari kilabu hiyo imepata motisha kufuatia ushindi wao wa mabao 3-0 dhidi ya kilabu ya West Ham siku ya jumamosi. .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni