Ajali ya Hiace imeua watu 24 eneo la Uwanja wa ndege Kiwila Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya.
Wadau katika eneo la tukio, mpaka sasa miili 22 imefanikiwa kutolewa. Kwani
Hiace hii ilidumbukia mtoni na bado miili miwili imenaswa, ndio inatolewa
muda huu. Watu
wawili tu ndio wamepona akiwemo kondakta. Ajali hii imetokea wakati
Coaster zinazofanya safari zake kati ya Mbeya na Kyela zikiwa kwenye mgomo hivyo
baadhi ya hiace za mjini kuamua kubeba abiria. Inaonekana ni ugeni wa
barabara, speed na gari kukosa breki za kuaminika.
Miili ya waliokufa ikingojea kupelekwa mochwari
Gari lililobeba Maiti likishusha Miili kuipeleka Chumba cha kuhifadhia Maiti.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni