Jumatano, 22 Aprili 2015

BAYERN YAZINDUKA, YAICHAPA FC PORTO 6-1, YASONGA KWA BAO 7-4

KAMA ULIFIKIRI BAYERN MUNICH WAMETOKA BAADA YA KIPIGO CHA MABAO 3-1 UGENINI URENO, BASI ILIJIDANGANYA. LEO WAMEITANGA FC PORTO KWA MABAO 6-1 NA KUFUZU HATUA YA NUSU FAINALI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA.
KATIKA MECHI HIYO YA MARUDIANO YA ROBO FAINALI TA LIGI YA MABINGWA ULAYA ILIYOPIGWA JIJINI MUNICH, WENYEJI HAO WALIPATA MABAO YAO KUPITIA KWA THIAGO ALCANTARA, ROBERT LEWANDOWSKI ALIYEFUNGA MAWILI, THOMAS MULLER, JEROME BOATENG NA XABI ALONSO WAKATI WAGENI WALIPATA BAO PEKEE KUTOKA KWA MARTNEZ.
MAANA YAKE MUNICH WAMEFUZU KWA JUMLA YA MABAO 7-4 DHIDI YA WARENO HAO. 







Hakuna maoni:

Chapisha Maoni