Akizungumza
na waandishi wa habari leo, Dr Mengi amesema ameshtushwa na taarifa
zinazomshutumu kuiangusha serikali ya Rais Kikwete.
Habari
hizo zilichapishwa na gazeti la 'TAIFA IMARA' likieleza mipango ya Mengi
kumwadabisha Rais JK hata baada ya kumaliza muda wake.
Mengi
amesema Rais alipewa taarifa hizo na Zitto Kabwe (kwa mujibu wa gazeti
hilo) na anashangaa kuona mpaka sasa Kurugenzi ya mawasiliano ikulu
haijakanusha.
Mengi
ameendelea kusema kuwa Rais ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote kwa hiyo
kutokanushwa kwa tuhuma hizo kunampa hofu ya maisha yake kwa sasa.
Chanzo: ITV habari!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni